Waziri wa
Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo
kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya
Ngongo, Manispaa ya Lindi tarehe 8 Agosti 2017.
Na
Mathias Canal, Lindi
Serikali
imesema kuwa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi itaendelea kuwa
muhimili na kichocheo katika kujenga uchumi wa viwanda ambao ndio kipaumbele
cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
Hayo
yalibainishwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Charles
Tizeba wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, nane nane
kitaifa, katika viwanja vya ngongo katika manispaa ya lindi tarehe
8/8/2017.
Dkt Tizeba
alisema kuwa kwa ushirikiano na Watumishi wote katika Wizara, amejipanga
kuhakikisha kuwa, Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaendelea kukua sawa sawa
na mahitaji ya Wananchi.
Alisema kuwa
jambo hilo linawezekana ambapo inawezekana kwa kiasi kikubwa kuzalisha
malighafi za kutosha za kuwezesha viwanda kuzalisha bidhaa mbalimbali, ambazo
zitauzwa ndani na nje ya nchi kwa bei nzuri na ya ushindani.
Alisema kuwa
kupitia mbinu hiyo wizara itakuwa imefanikisha kuongeza mchango wa Sekta hizo
katika uchumi wa Taifa na pia katika kuondoa umaskini kwa Watanzania wengi.
Sambamba na
hayo pia Mhe Dt Tizeba alisema kuwa Sekta ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, mabadiliko ya tabianchi,
ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao,
uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji.
Katika
kukabiliana na jambo hilo Mheshimiwa Dkt Tizeba alisema kuwa Wizara yake
imejipanga kuendelea, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi,
ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora zinazovumilia ukame, magonjwa na kutoa
mavuno mengi.
Alisema kuwa
Serikali kwa kushirikiana na Wabia wa Maendeleo, wamekamilisha Mpango wa Kilimo
Kinachohimili Mabaliliko ya Tabianchi na Miongozi ya uzalishaji mazao, ufugaji
na uvuvi. Muongozo wa kilimo umetolewa kulingana na Kanda za Kilimo za
Kiteknolojia. Miongozo hiyo, imezinduliwa na kuanza kusambazwa kwa Maafisa
Ugani wa Kilimo Mifugo na Uvuvi na kwa wananchi, kuanzia Mwezi, Mei na Juni,
2017.
Alisema
Mikakati mingine, inayoendelea ni pamoja na kuhakikisha kuwa mbolea bora,
inapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu zaidi, sawasawa na agizo la Makamu wa
Rais la kuwasaidia Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kupunguza gharama za uzalishaji
ili waweze kufaidika na matunda ya juhudi zao.
Sambamba na
hilo aliongeza kuwa wizara yake imejipanga ili kuhakikisha kuwa inaendelea
kuwaelimisha na kuwasaidia Wafugaji wa Tanzania, kufuga kitaalamu zaidi ili
kuepuka hali ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho na maji.
Alisema kuwa
jambo hilo litawezesha kufuga kwa tija na pia kupunguza migogoro ya Wakulima na
Wafugaji.
|
No comments:
Post a Comment