Nukuu ya JPM-“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe”. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 11, 2017

Nukuu ya JPM-“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe”.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema anazipenda Taasisi zinazofanya kazi ya kuonekana na sio zinazoongea ongea.
Akihutubia hapo  Jana July 10, 2017 katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation zitakazotumika katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera, Rais Magufuli licha ya kuipongeza Taasisi ya Mkapa akisema…“Mimi nazipenda sana Taasisi zinazofanya kazi kama hii ya Mkapa Foundation sio zinazotaka watoto wazae wakiwa shule. Taasisi za kila siku kwenye majukwaa mzinyime fedha, nataka Taasisi zinazofanya kazi inayoonekana sio za kuongea ongea tu.

Hata mimi yupo mtoto wa mdogo wangu amezalia nyumbani, mtoto anamuita John, wa pili anamuita Samia lakini hakubakwa. Tunafanya ukaguzi nchi nzima kuwajua waliotumia vibaya fedha za pembejeo ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.5.” – Rais Magufuli.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.

Post Bottom Ad