Ronaldo Mcheza Soka Bora wa Dunia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 10, 2017

Ronaldo Mcheza Soka Bora wa Dunia.

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA.
Akizungumza baada ya kushinda tuzo hiyo mjini Zurich, Ronaldo alisema: "Kama nilivyowahi kusema mara nyingi, mwaka jana ulikuwa mwaka wa ndoto. Real Madrid ilishinda Ligi ya Mabingwa, na Ureno ubingwa wa Ulaya. Ninajivunia na nina furaha sana, na ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa mwaka mzuri,"alisema.

 Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.

Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d'Or mwezi Disemba mwaka jana 2016, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya Taifa ya Ureno.

Ronaldo kwa mara ya kwanza aliibuka na mpenzi wake mpya, Georgina Rodriguez baada ya tetesi za kwamba wapo kwenye mahusiano.

Ronaldo aliisaidia Real Madrid kubeba Ubingwa wa Ulaya lakini akaisaidia Ureno Picha chini kubeba ubingwa wa Ulaya kwenye EURO 2016 nchini Ufaransa.

Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Carli Lloyd wa USA.

Kocha Bora Duniani kwa Wanaume ni Claudio Ranieri baada ya kuiwezesha Leicester City, bila kutegemewa, kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia yao.

Nae Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia ndie alitwaa Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka.

Kwenye Tuzo ya Mashabiki, Mashabiki wa Timu za Liverpool na Borussia Dortmund, kwa pamoja, wameshinda Tuzo hii kwa tukio la kuimba wote ‘Wimbo wa Taifa wa Liverpool’ -'You'll Never Walk Alone'- Uwanjani Anfield kabla ya Mechi yao ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita.

FIFA TUZO ZA UBORA – WAGOMBEA NA MSHINDI.
MCHEZAJI BORA WANAUME:
-Wagombea: Cristiano Ronaldo, Antoine Griezmann, Lionel Messi
-Mshindi: Cristiano Ronaldo
MCHEZAJI BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Melanie Behringer, Carli Lloyd, Marta
-Mshindi: Carli Lloyd wa USA.
KOCHA BORA WANAUME:
-Wagombea: Claudio Ranieri, Fernando Santos, Zinedine Zidane
-Mshindi: Claudio Ranieri wa Mabingwa wa England Leicester City
KOCHA BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Jill Ellis, Silvia Neid, Pia Sundhage
-Mshindi: Silvia Neid [Germany]
GOLI BORA [Tuzo ya Puskas]:
-Wagombea: Marlone, Daniuska Rodriguez, Mohd Faiz Subri
-Mshindi: Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia.
**Tuzo hii inatokana na Kura za Mashabiki Duniani kote.
TUZO TOKA KWA MASHABIKI:
-Wagombea: Mashabiki wa Den Haag, Borussia Dortmund & Liverpool na Iceland.
-Mshindi: Mashabiki wa Borussia Dortmund & Liverpool
TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI
-Mshindi: Atletico Nacional ya Colombia
FIFA FIFPro World11 2016 – Kikosi Bora cha Mwaka 2016:
-Kipa: Neur
-Mabeki: Alves, Pique, Ramos, Marcelo
-Viungo: Modric, Kroos, Iniesta
-Mafowadi: Suarez, Ronaldo, Messi
++++++++++++++++++++++++++
KURA KUPATA WASHINDI:
-Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:
-Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA
-Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki

-Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad