UHALIFU / PICHA:- Majambazi yenye Silaha za Moto Yapora mil 6/- kwa Mfanyabiashara wilayani Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 07, 2016

UHALIFU / PICHA:- Majambazi yenye Silaha za Moto Yapora mil 6/- kwa Mfanyabiashara wilayani Ngara.


Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiwasalimia wananchi WA eneo la Benaco wilayani Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi, 2016..Picha Kutoka Maktaba yetu.. 

Majambazi waliokuwana na  silaha za moto wamevamia  na kuiba fedha na Simu Dukani kwa Mfanyabiasha wa Miamala ya Fedha ( M PESA )  lililopo Mji mdogo wa Benako wilayani Ngara,Mkoani Kagera na kupora Sh milioni 6 za Kitanzania na elfu 40.

Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara Bw Muhamed Kipano amesema tukio hilo limetokea jana, July 06, 2016, majira ya saa mbili usiku.

Amemtaja mfanyabiashara aliyevamiwa kuwa ni Bw Nicholas Fortunatus ambaye ameibiwa Shilingi  Milioni 4 na Elfu 40 taslimu pamoja na Simu iliyokuwa na Shilingi Milioni 2 za M-PESA kwenye akaunti.

Kabla ya kutekeleza tukio hilo, majambazi hao walifyatua risasi 7 hewani mfululizo na kwamba hadi sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa na upelelezi unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad