PICHA / VIDEO: Jeshi la Polisi Laelezea Chanzo cha Ajali ya Mabasi ya City Boys Mkoani Singida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 06, 2016

PICHA / VIDEO: Jeshi la Polisi Laelezea Chanzo cha Ajali ya Mabasi ya City Boys Mkoani Singida.

July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 54 ambapo hadi leo wamebaki majeruhi 33 wakiendelea na matibabu. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga amesema

>>>’kwa ajali iliyotokea Maweni Singida siyo ajali ya kawaida bali ni tukio la kufanya mauaji bila kukusudia, hivyo polisi imedhamiria kuwafikisha mahakamani madereva waliohusika na ajali hiyo kwa mashtaka ya mauaji bila kukusudia kutokana na taarifa za awali za chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo ni kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.

>>>Aidha tumewasiliana na wenzetu wa SUMATRA, kampuni ya mabasi ya City Boys na makampuni mengine yaliyohusika katika ajali yafungiwe kutoa huduma za usafirishaji katika njia zote hapa nchini....HAPA CHINI BOFYA KUMSIKILIZA KAMANDA MPINGA NA TAARIFA JUU YA AJALI HIYO.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad