|
Mmoja wa Madereva
waliosababisha ajali ya mabasi ya City Boy, Jumatatu iliyopita ya Julai 04,2016 katika kijiji cha
Maweni wilayani Manyoni, Jeremiah Semfungwe (34), amefikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na makosa 30 ya kuua bila kukusudia.
Mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, ilidaiwa kuwa mshitakiwa Semfungwe
alitenda makosa hayo Julai 4 mwaka huu saa 8.15 mchana wakati akiendesha basi
T. 247 BCD mali ya Kampuni ya City Boy kwa kuligonganisha na basi T. 331 DCE.
Wakili Mkuu Mfawidhi wa
Serikali, Zakaria Ndaskoi alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa ambaye ni Dereva
na mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, bila kukusudia, alisababisha vifo
vya abiria 30 kinyume na Kifungu 195 na 198 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16
Toleo la Kwanza.
|
No comments:
Post a Comment