TASWIRA PICHA:-JPM….’'Nimekaa Serikalini kwa miaka 20, kuwekeana wivu Mtanzania akitaka kuwekeza kupo sana, tumeamini watu kutoka nje kuliko sisi wenyewe'’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2016

TASWIRA PICHA:-JPM….’'Nimekaa Serikalini kwa miaka 20, kuwekeana wivu Mtanzania akitaka kuwekeza kupo sana, tumeamini watu kutoka nje kuliko sisi wenyewe'’

.

Rais Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini, Waziri Mwijage, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na Mwenyekiti wa CTI Samuel Nyantahe.
2

Rais Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka Viwandani.
6

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alialikwa katika hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo,May 31, 2016, Jijini Dar es Salaam.



Rais Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kuwa serikali yake itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wenye viwanda na wenye nia ya kuanzisha viwanda vipya ili kufanikisha nia yake ya kuzalisha ajira nyingi, kukuza uchumi na kuiwezesha serikali kukusanya mapato zaidi.



Hizi ni sentensi tano alizozizungumza Rais Magufuli kwenye hotuba yake….



    'Nimekaa serikalini kwa miaka 20, kuwekeana wivu Mtanzania akitaka kuwekeza kupo sana, tumeamini watu kutoka nje kuliko sisi wenyewe' – JPM



    'tuweke nguvu kubwa kwa wanachi kuwa na viwanda, nataka niwathibitishie nawapenda wafanyabiashara wenye nia nzuri ya kuanzisha viwanda'-JPM

    'Aina ya viwanda tunavyolenga kwa kiwango kikubwa ni vya uzalishaji ambavyo hutumia malighafi zinazopatikana kwa wingi ndani ya nchi' -JPM



    'Nataka Nchi ya Viwanda halafu pawepo mtu anakwamisha ataondoka, nimezunguka nchi nzima nasema nataka nchi ya viwanda sikuwa kichaa' -JPM
7 7b 8 1
7 2..

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad