fastjet-a319-100-12.jpg?zoom=1
Hali kadhalika ilianzisha safari za Kimataifa  kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya,  Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli zake.

Tangu tuanze safari zetu  tumeshabeba abiria zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa  zaidi ya theluthi moja  ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza kumudu  kusafiri kwa ndege”, anasema Corse.

Aliendelea kusema, “kuongeza ndege  nyingine  kwenye safari zetu  kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa  njia zetu zilizopo  ili kukidhi mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.

Hali kadhalika, Corse anabainisha kuwa ndege hiyo mpya  inamanisha kuwa fastjet ni sawia na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.

Ndege hiyo A319  ambayo ni Airbus  ni ya injini mbili  ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni nyongeza kwenye  viwango vya juu vya hali ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba  abiria  156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet Tanzania.

Baadhi ya  njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya itakuwa inahudumia  ni njia mpya iliyoanzishwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na Nairobi  na Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya  zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye upanuzi wa  njia za fastjet kitaifa na kimataifa.

Fastjet inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya  kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali kadhalika  imeshajionesha kuwa kuna matarajio ya  kuzindua  safari kati ya Zanzibar na Nairobi  na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.

Usafiri wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye  kukuza uchumi wa Tanzanoa, hususani kwenye   kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema Corse.

Hali kadhalika Corse alibainisha kuwa ndege hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji  iwapo  ndege moja miongoni mwake itakuwa haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.


ata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630-/+255756830214.