Ligi Kuu
soka Uingereza 2015/2016 imeendelea tena usiku wa December 29,2015 kwa mchezo mmoja
kupigwa katika dimba la King Power, Kati ya Leicester City dhidi ya klabu ya Manchester
City.
Matokeo ya
mchezo huo ulimalizika kwa kutoka 0-0.
Kila Timu
ilipata nafasi kupitia mashine zao za Magoli, Jamie Vardy kwa Leicester na
Sergio Arguero kwa City, lakini wakapoteza.
Matokeo haya
yaneifanya Leicester wafungane kwa Pointi na Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza wote wakiwa na Pointi 39 lakini Arsenal ndio Vinara kwa Ubora wa
Magoli.
Man City ni
wa 3 na wako Pointi 3 nyuma.
Leo December
30,2015 ipo Mechi 1 pekee ya Ligi ya kufunga Mwaka huko Stadium of Light kati
ya Sunderland na Liverpool.
Papo kwa Papo >>>>Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER, INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
No comments:
Post a Comment