EPL 2015/2016:-Manchester United yapigwa 2 – 1 na Kukamilisha wiki ya Machungu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 13, 2015

EPL 2015/2016:-Manchester United yapigwa 2 – 1 na Kukamilisha wiki ya Machungu.

Manchester United wamehitimisha wiki ya machungu, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza jana December 12,2015, usiku wakiwa Uwanja wa Vitality.

Mabao ya Bournemouth yamefungwa na Junior Stanislas dakika ya pili na Joshua King dakika ya 54, wakati la Man United limefungwa na Marouane Fellaini dakika ya 24.

Kipigo hicho kinakuja baada ya Manchester United kutolewa katoka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015/2016 katikati ya wiki, baada ya kufungwa mabao 3-2 na VfL Wolfsburg nchini Ujerumani.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad