BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA:-Rais Magufuli ‘amaliza kazi’. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 27, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA:-Rais Magufuli ‘amaliza kazi’.

Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea ofisini kwake Dar es Salaam jana November 26,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Ofisi ya Waziri Mkuu ilithibitisha Dk Magufuli kutinga ofisini kwa Waziri Mkuu, Majaliwa na kufanya mazungumzo ya takribani saa moja.

Rais aliingia ofisini kwa Waziri Mkuu Majaliwa majira ya saa tisa na kulakiwa na mwenyeji wake na baadaye walikaa kwa mazungumzo yao wawili tu. “Baada ya mazungumzo hayo, Rais alizungumza kwa muda mfupi sana na makatibu Muhtasi wa Waziri Mkuu kabla ya kuondoka kuelekea Ikulu,” ilieleza taarifa fupi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Rais wa Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania,Dr. John Magufuli ambaye tangu Novemba 17, mwaka huu 2015,alikuwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa majukumu mbalimbali, amerejea Dar es Salaam jana,November 26,2015 na wakati wowote inaelezwa kwamba anaweza kutangaza Baraza la Mawaziri linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania.

Dk Magufuli alitua Ikulu ya Chamwino, Novemba 17 kwa kutumia usafiri wa barabara akisafiri kwa zaidi ya kilometa 300 kwenda katika Makao Makuu ya Serikali ambako kwanza alikuwa na majukumu mawili makubwa.

Novemba 19, mwaka huu, alimteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu na siku iliyofuata alimwapisha katika Ikulu hiyo iliyoko takribani kilometa 40 kutoka Dodoma Mjini.
Aidha, baada ya kumwapisha Majaliwa asubuhi, jioni hiyo ya Novemba 20, Dk Magufuli aliyeingia madarakani Novemba 5, mwaka huu 2015, alilihutubia na kulizindua Bunge la 11 mjini Dodoma katika hotuba iliyosisimua wabunge na Watanzania kwa ujumla kwa kugusa kero na mipango mbalimbali anayokusudia kuifanya.

Dk Magufuli alirejea Dar es Salaam huku tetesi zikiimarika kwamba atatangaza baraza lake la mawaziri siku yoyote kuanzia jana November 26,2015, na aliondoka Dodoma kwa ndege majira ya saa mbili asubuhi.

Kuwapo kwake kwa siku nyingi katika kijiji cha Chamwino akifanya kazi, kulipongezwa na wanakijiji hao. Aidha, wanazuoni na wanasiasa walitafsiri uwapo wake kijijini hapo kuwa ni kujichimbia asibughudhiwe wakati akipanga baraza lake la mawaziri na mfumo wa uendeshaji mpya wa baraza hilo.

Na ishara au dalili kwamba Baraza la Mawaziri limeiva au litatangazwa wakati wowote ni hatua ya Dk Magufuli kutua Dar es Salaam na baadaye mchana kwenda ofisini kwa Majaliwa ambako ni jirani na Ikulu ya Magogoni.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Rais atateua Baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, hivyo kuna kila dalili wawili hao kama sio wote watatu, wameshafanya kazi hiyo. SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA

 
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad