VPL 2015/2016:-Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara,Msimamo na Ratiba yake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 23, 2015

VPL 2015/2016:-Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara,Msimamo na Ratiba yake.

Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea tena jana October 22,2015  kwa michezo minne kupigwa katika viwanja vinne,  na Azam FC wameikamata Yanga SC kileleni kwa Pointi baada ya kuifunga Ndanda FC Bao 1- 0.

 Bao pekee la Azam FC lilifungwa Dakika ya 70 na Shomari Kapombe kwenye Mechi iliyochezwa huko Nangwanda Mtwara.

Ushindi huu umewafanya Azam FC wafikishe Pointi 19 sawa na Vinara Yanga SC lakini wao wanakaa Nafasi ya Pili kwa vile Yanga SC wana goli nyingi.

Huko Mwadui, Shinyanga, Wenyeji Mwadui FC wameichapa Mgambo Shooting Bao 3-1 kwa Bao 2 za Jerry Tegete na Jamal Mnyate huku Abuu Daudi akiwapa Mgambo Bao lao pekee.

Kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, JKT Ruvu ilitoka 0-0 na Mtibwa Sugar wakati huko Sokoine, Mbeya, Bao la Geofrey Mlawa limewapa Mbeya City ushindi wa Bao 1-0.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016 MATOKEO

Jumatano Oktoba 21,2015.

Yanga SC 4 – 1 Toto Africans 

Stand United 3 – 0 Majimaji FC

Tanzania Prisons 1 – 0 Simba SC

Coastal Union 1 – 0 Kagera Sugar


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad