Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na Alhaj Aliko Dangote
wakifunua pazia kuashiria kuzindua rasmi
kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya
saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.
Inaelezwa kuwa
Kiwanda hicho kitatoa ajira 1,500 za moja kwa moja sambamba na vibarua 9,000.
Kwenye list
ya Matajiri wakubwa wanaotambulika Duniani kwa sasa yuko pia mfanyabiashara
Alhaji Aliko Dangote ambaye ni Raia wa Nigeria, Afrika anatajwa kuwa tajiri wa
kwanza kabisa.
Utajiri wake
unatokana na nguvu kubwa ambayo amewekeza kwenye Biashara na Miradi mbalimbali
ikiwemo Miradi ya Sukari, Cement, Mafuta na Biashara nyingine kubwakubwa.
Alikuja
Tanzania pia akahitaji kuwekeza moja ya Miradi yake mikubwa, akapata ruhusa ya
kufanya ujenzi wa Kiwanda cha Cement Mtwara.
|
No comments:
Post a Comment