TASWIRA PICHA:- Mkuu wa Mkoa wa Kagera ashiriki zoezi la kutoa Mahindi ya Msaada wilayani Karagwe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 23, 2015

TASWIRA PICHA:- Mkuu wa Mkoa wa Kagera ashiriki zoezi la kutoa Mahindi ya Msaada wilayani Karagwe.

Mkuu  wa  Mkoa  wa  Kagera ,Bw. John  Mongella  (mwenye kofia ) ameshiriki  zoezi  la  kuwagawia  mahindi  yaliyotolewa  na  Serikali  kwa  wahanga   wa  maafa  ya mvua  zilizonyesha zikiambatana  na  upepo  mkali  na  kusababisha  madhara  makubwa  kwa  kata  za  Kanoni, Igurwa  na  Kihanga  zilizonyesha  Agosti 31  mwaka  huu  2015, ambapo  serikali  imetoa  tani  40  za  mahindi.
Akitoa  neno  kwa  wananchi  hao  ambao  ni  wahanga  wa  maafa  hayo  kabla  ya  kushiriki  zoezi  la  kuwagawia  mahindi  wananchi  mkuu  wa  Mkoa  wa  Kagera  amesema  kuwa   serikali  itaendelea  kuwajali  wananchi  wake  kwa  wakati  wowote  ule  pindi  majanga  yanapojitokeza  kwani  siku  zote  serikali  ipo  kwa  ajili  ya  kuwasaidia    wananchi  wake.
Amesema  zoezi  hilo  la  kutoa  msaaada  wa  chakula  kwa  wahanga  hao  lisihusishwe  na  kampeini  za  vyama  vya  siasa  zinazoendelea  kwa sababu  hakuna  anayeomba  maafa  yatokee  ili  anayeomba  kura  aitumie  kama  fursa  ya  kujipatia  umaarufu  au  kura.
Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Deodatus  Kinawiro   awali akisoma  taarifa  ya  wilaya  amesema  kuwa kata zilizoathiriwa  na  mvua  hizo  zilizonyesha  Agosti 31 na  Septemba 3  mwaka  huu,2015 kuwa ni kata  za Kihanga, Kanoni, Igurwa  na  sehemu  ndogo  ya  Kata  ya  Bugene  amesema  wilaya  ya  Karagwe  walikuwa  wameomba   kupatiwa  tani  48  za  mahindi  lakini  wamepatiwa  tani  40    na  tani  16  za  maharage  walizokuwa  wameomba  hazikuweza  kupatikana.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad