MATOKEO UCHAGUZI MKUU 2015:-Yaliyotangazwa Rasmi Bukoba Mjini,Karagwe,Kahama na Kigoma mjini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 26, 2015

MATOKEO UCHAGUZI MKUU 2015:-Yaliyotangazwa Rasmi Bukoba Mjini,Karagwe,Kahama na Kigoma mjini.

JIMBO LA BUKOBA

Pamoja na Hali ya taharuki kutanda katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera baada ya Jeshi la Polisi kuanza kufyatua  mabomu ya machozi pamoja na Maji ya kuwasha ili kuwatawanya mamia ya wakazi wa Jimbo la Bukoba Mjini wanaoshinikiza kutangaziwa matokeo ya ubung.

 Wananchi wameonekana wakisubiri matokeo hayo tangu asubuhi baada ya kupata matokeo ya awali yaliyoonesha kuwa Mgombea kupitia CHADEMA, Bw Wilfred Rwakatare anaongoza kwa kura 28,112 dhidi ya Mgombea wa CCM Balozi Hamis Kagasheki aliyekua na kura 25,565.

Hadi sasa wananchi, waandishi wa habari pamoja na waangalizi wa Uchaguzi huo wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi huo ngazi ya Ubung.

JIMBO LA KARAGWE

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe Mkoani Kagera kupitia Chama cha Mapinduzi Bw Innocent Bashugwa ametangazwa kuwa mshindi ambapo akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi wilayani Karagwe Bw Richard Ruyango amesema Bw Bashungwa amewashinda wagombea watatu kutoka Chadema, TLP na UDP baada ya kupata kura elfu 57 na 322 sawa na asilimia 54.92
Kwa upande wake Bw Bashungwa amewashukuru wakazi wa Karagwe kwa kumuamini na ambapo ameahidi kuwatumikia kikamolifu kwa kutekeleza vipaumbele vyakeikiwemo Elimu, Afya na Barabara

JIMBO LA KIGOMA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo Bw Zitto Kabwe ametangazwa kuwa Mshindi wa nafasi hiyo

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi uliofanyika jana October 25,2015, Msimamizi wa Uchaguzi katika Manispaa hiyo Mhandisi Bonipace Nyambele amesema jimbo hilo mgombea huyo ameshinda nafasi hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wagombea kumi na sita jimboni humo

Mhandisi Nyambele amesema Bw Zitto amepata kura Elfu 31 na 546 kati ya kura Elfu 91 na 824 zilizopigwa.
Bw Kabwe amefuatiwa na Dr Aman Kaburu kupitia CCM aliyepata kura Elfu 17 na 314 huku Bw Daniel Lumenyera kupitia Chadema kipata Kura Elfu 12 na 77

Bw Zitto Kabwe amesema atahakikisha anafanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kulifanya jimbo hilo kuwa mfano kimaendeleo hapa nchini

JIMBO LA KAHAMA

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Bw Jumanne Kishimba ametangazwa kuwa Mshindi dhidi ya Bw James Lembeli wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema

Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Kahama Mjini Bw Anderson Msumbwa amesema Bw Kishimba ameshinda kwa kura Elfu 47 na 555 akifuatiwa na Bw Lembeli aliyepata kuta elfu 30 na 122  huku Bw Bobson Wambura awa ACT Wazalendo akipata Kuta 605

Amesema katika Jimbo la Kahama mjini lililokuwa na wapiga Kura Laki Moja Elfu 49 na 344 waliokuwa wamejiandikisha huku watu elfu 78 na 280 wakijitokeza kupiga kura, hakukuwa na kura iliyoharibika.

Bw Msumbwa amesema katika uchaguzi huo jimbo la Kahama mjini lilikuwa na vituo 321 vya kupigia kura katika kata 20 na kwamba katika matokeo ya udiwani, Chama cha Mapinduzi kimepata madiwani 19 na Chadema kimepata kiti kimoja.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad