KAMPENI URAIS CCM 2015:- Taswira Picha za mkutano wa Mgombea ,Dr John Magufuli – Lindi October 12,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 13, 2015

KAMPENI URAIS CCM 2015:- Taswira Picha za mkutano wa Mgombea ,Dr John Magufuli – Lindi October 12,2015.


Ziara za wagombea nafasi za Urais kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania bado inazidi kuchukua kasi,upande wa Chama Cha Mapinduzi na mgombea wake John Magufuli alizungumza  na wakazi wa Lindi hapo jana October 12,2015 ambapo aliwataka Watanzania wametakiwa kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu na kumchagua kiongozi muadilifu atakayeweza kuzisimamia kikamilifu maliasili na rasilimali za taifa ili Tanzania iweze kupiga hatua za haraka za kimaendeleo kwa faida ya watanzania wote bila ya kujali matabaka yao ya kijamii kwa kuangalia rekodi ya utendaji ya viongozi wanaotaka ridhaa ya watanzania kuongoza nchi.

Dr John Pombe Magufuli ameahidi kufanya kazi kwa lengo la  kupunguza changamoto za kimaisha zinazowakabili watanzania kutokana na kukosa uadilifu na uaminifu pia utayari wa kuwatumikia watanzania licha ya uwepo wa rasilimali na maliasili lukuki ambazo Tanzania imekirimiwa na muumba wetu...Picha zote kwa hisani ya MILLARDAYO.COM

2
Ali Kiba na wacheza show wake wakishambulia jukwaa kwenye viwanja vya Sokoni Majengo kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

27
Mkwe wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mama Salma Kikwete akihutubia wakazi wa Lindi mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za uliofanyika kwenye viwanja vya Mpilipili.

22
Dr Magufuli amefanya mikutano katika majimbo ya Nachingwea, lwangwa na Mtama pia Lindi mjini katika viwanja vya Mpilipili mkutano uliohudhuriwa na mke wa rais mama Salma Kikwete, Waziri wa mambo ya nje Mh Bernard Membe pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali ambapo watanzania wametakiwa kupuuza habari za uzushi zinazotolewa na baadhi ya wagombea.

17
Mgombea ubunge jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akihutubia mbele ya Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni Majengo.
12
Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha ilani ya CCM mgombea ubunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni Majengo

7
Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mtama mkoani Lindi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni Majengo.

9
11
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad