SHERIA / TEKNOLOJIA:-Zifahamu Tochi ( SPEED RADAR ) ambazo we Dereva jiandae kukutana nazo huko Barabarani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 01, 2015

SHERIA / TEKNOLOJIA:-Zifahamu Tochi ( SPEED RADAR ) ambazo we Dereva jiandae kukutana nazo huko Barabarani.

Tochi hizi za kisasa kabisa zimesambazwa 400 mikoa yote ya Tanzania hivyo kila mkoa unatochi kadhaa za teknolojia hii mpya. Kwa hiyo jiandae kukutana nazo huko Barabarani.
MAELEZO KUHUSU VITU VINAVYOONEKANA KATIKA PICHA ZA TOCHI ( SPEED RADAR) NA UWEZO WA TOCHI HIZI.

1. Alama ya sifuri

Tunaambiwa alama hii haina maana yoyote zaidi ya kuwepo tu hapo, sana sana inasaidia kulenga target tu ya gari ambalo askari anataka kulipima mwendo. Alama hiyo ingeweza kuwa x,z au yoyote ile.

2. Baadhi ya picha speed inaonekana kwa kutanguliwa na alama ya hasi (negative) mfano -30;-107 nk.

Hii inamaanisha kuwa gari hiyo imepimwa kutoka nyuma. kimsingi ilipita kwa askari kwa speed sahihi lakini baada ya kumpita askari ikaongeza mwendo ikiwa bado kwenye eneo la 50 au 30. Hilo ni kosa bado gari hili litachukuliwa hatua.

3. Speed isiyo na alama ya negative mf. 107, 65 nk

Hii inamaanisha gari imepimwa kutoka mbele, yaani kadiri inayokuja upande wa askari, kama ambavyo tochi za kawaida za zamani zimekuwa zikipima.



4. Memory.

 Tochi hizi zina memory hadi 64GB na haziruhusu askari kufuta akiwa field.

5. Uchaguzi wa gari.

Zikiwepo gari tano mfano zinakuja Askari ana uwezo wa kuchagua ni gari gani aipime, sio lazima ya mbele tu, ili mradi hiyo point 0 ailenge kwenye gari husika.

6. Umbali wa kupima.

Tochi hii mpya inaweza kupima umbali kuanzia mita 3 hadi mita 1829 yaani umbali zaidi ya kilomita moja na nusu(1.5km).


Elimu hii kwa hisani ya :-Fungo Augustus /RSA.


PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad