![]() |
Afisa Uhusiano
wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’
itakayomwezesha mteja kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi
(SMS) bila kikomo pamoja na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango
cha shilingi 300 tu. Kushoto ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio
Kaniki.
“Yatosha Nyts” inawawezesha
wateja kuwasiliana na familia, marafiki, mpenzi na wafanya biashara wenzao
wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.
Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni
mwendelezo wa kutoa huduma za mawasiliano bora zenye gharama nafuu, wateja
wetu wanauwezo wa kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza
kufurahia kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi kwa shilingi
300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel kwenda
Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao yote na 10
MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku.
![]() |
Kujiunga na
“Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya na moja kati ya ofa
nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja wake chini ya huduma ya
kibunifu ya Airtel Yatosha. Airtel
Yatosha inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia
huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma. Yatosha pia
inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na
ya kwanza kutoka Airtel.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment