KAMPENI UKAWA 2015:-Mbowe alivyosindikizwa na Lowassa, Mbatia kwenye uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la HAI. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 27, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:-Mbowe alivyosindikizwa na Lowassa, Mbatia kwenye uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la HAI.

Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 zimeendelea Tanzania, leo nakusogezea hii kutoka Jimbo la Hai Mkoa wa Kilimanjaro.. Mbunge anayemaliza muda wake Freeman Mbowe amefika leo Jimboni kwake na kuzindua Kampeni zake za kugombea Ubunge kwa mara nyingine, wapo waliomsindikiza pia !!

Mgombea Urais kupitia CHADEMA na Umoja wa Vyama vya UKAWA, Edward Lowassa na wengineo ikiwemo James Mbatia walikuwepo kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo.


DSC_9983

DSC_9806
DSC_9823
DSC_9837
Huku akionekana kujiamini kushinda katika chaguzi ujayo, Freeman Mbowe (pichani) anayewania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la hai amewataka wanahai na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.
DSC_9860
DSC_9865
DSC_9878
Fredrick Sumaye ( Pichani ) ambaye ni Waziri mkuu mstaafuakihutubia maelfu wakazi wa jimbo la hai amesema ni wakati muafaka wa kukiondosha chama cha CCM madarakani kwani kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na kufanya nchikuendelea kuwa masikini.
DSC_9891
Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi nchini UKAWA Edward Lowasa, ameahidi kuhakikisha  anapambana na tatizo la rushwa ambalo limekuwa chanzo cha umasikini nchini.

Siku 29 pekee kuelekea octobar 25 mwaka huu,2015, sauti bado ni ile ile kila kona ya nchi akiwa mjini hai ambapo alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Lunongai, Shirimatunda, Machame na Hai mjini, Edward Lowasa amesema atahakikisha anaongoza nchi kwa misingi ya haki na usawa hukua kiahidi kutumia vema ilani ya ukawa kuhakikisha anapambana na rushwa  kwani kwa muda mrefu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi huku wachache wakinufaika na rasilimali za nchi.
DSC_9924
DSC_9959
DSC_9609
DSC_9633
DSC_9644
DSC_9655
DSC_9670
DSC_9692
DSC_9746
DSC_9754
DSC_9765
DSC_9771
DSC_9786
DSC_9801
Mama Regina Lowassa.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad