UFAHAMU:- TFDA yavifunga viwanda vitano vya vipodozi Kisa kubainika kutengeneza krimu, losheni na jeli zenye viambato sumu aina ya ‘steroid’. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 18, 2015

UFAHAMU:- TFDA yavifunga viwanda vitano vya vipodozi Kisa kubainika kutengeneza krimu, losheni na jeli zenye viambato sumu aina ya ‘steroid’.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA Dar es Salaam jana August 17,2015, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu.
 Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Huduma wa TFDA, Chrispin Severe .
 Mkurugenzi wa Usalama wa chakula, Raymond Wigenge (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Charys Ugullam (kulia), wakiwa kwenye mkutano huo na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

1.            MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2.            TFDA inautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kwenye soko, imebaini uwepo wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku aina ya “steroids” zinazojulikana kitaalam kama “clobetasol propionate”, “hydrocortisone” na “triamcinolone”.

3.            Jumla ya Vipodozi aina tofauti 36 vya jamii ya krimu (creams) na losheni (lotion) vimebainika kuwa na viambato hivyo vilivyopigwa marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vilivyotengeneza.

4.            Vipodozi hivyo vimetengenezwa na makampuni manne (4) yaliyoko hapa nchini na kiwanda kimoja (1) kilichoko nje ya nchi kama ifuatavyo:-

Na.
Jina la kiwanda
Idadi ya vipodozi
Idadi ya matoleo
1.
Chemi & Cotex Industries Limited - Dar es Salaam
6
7
2.
Mamujee Products Limited - Tanga  
11
20
3.
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited - Tanga
15
24
4.
Tridea Cosmetics Limited - Dar es Salaam
3
5
5.
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London, South Africa
1
1
Jumla
36
57


5.            Steroids aina ya “clobetasol propionate”, ‘hydrocortisone’’ na “triamcinolone” hutumika kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yajulikanayo kitaalam kama eczema, herpes labialis, psoriasis, contact dermatitis, alopecia areata, vitiligo, lichen sclerosus, lichen planus na mycosis fungoides. Steroids hizi hazitakiwi kutumika zaidi ya wiki mbili na lazima mgonjwa apate ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi.

6.            Baadhi ya madhara yanayotokana na kutumia dawa hizi ni pamoja na muwasho na kuvimba kwa ngozi (allergic contact dermatitis), ngozi kuwaka moto (burning sensation), ngozi kukatikakatika (skin cracking), ngozi kubabuka (fissuring) ngozi kukosa chembembe aina ya melanin inayoleta kinga na hivyo kuifanya ngozi kuwa nyeupe isivyo kawaida (hypopigmentation), madhara kwenye mifupa (osteoporosis), kizunguzungu (dizziness), ngozi kukauka (skin dryness), shinikizo la damu kwenye macho (glaucoma), vinyweleo vya ngozi kupata athari (folliculitis), kuwashwa mara kwa mara (excessive itching, pruritus, erythema and irritations), vidole kufa ganzi (numbness of fingers), ngozi kusinyaa (skin atrophy) na ngozi kubanduka (skin peeling/maceration). 

 Madhara mengine ni pamoja na ngozi kuwa nyekundu (skin redness), kusikia kichefuchefu (nausea), kichwa kuuma (headache), kushindwa kupata usingizi (insomnia), kutoka jasho jingi (sweating), kupata chunusi kubwa kwenye ngozi (acne), kuchoka (fatigue), kuongezeka uzito (weight gain), mapigo ya moyo kutoenda sawa (uneven heartbeats) na kuona maluweluwe (blurred vision). 

7.            Kufuatia hali iliyojitokeza na kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya steroids kwa muda mrefu, TFDA imechukua hatua zifuatazo:-

a.      Kuzuia kwa muda wa miezi sita (6) utengenezaji wa vipodozi aina ya krimu, losheni na jeli kwenye viwanda vinne (4) vilivyohusika. 
b.      Kuwaelekeza wenye viwanda vilivyohusika kuviondoa vipodozi vilivyokutwa na steroids kwenye soko na kuviteketeza kwa gharama zao wenyewe.
c.       Kufuta usajili wa vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
d.     Kuwaelekeza Mameneja wa Ofisi za Kanda za TFDA kufanya ukaguzi katika maeneo yao kwa kushirikiana na Ofisi za Halmashauri ili kuondoa katika soko vipodozi vyote vilivyohusika.

8.            Pamoja na hatua hizo, TFDA inatoa maelekezo yafuatayo:-

a.      Wananchi wote wasitumie vipodozi husika kwa kuwa vina madhara ya kiafya. Wananchi wanaaswa kuangalia lebo za vipodozi walivyonavyo majumbani na wakiona vina majina yaliyoainishwa waache kutumia vipodozi hivyo mara moja.
b.      Wasambazaji na wauzaji wote kurudisha vipodozi vilivyohusika kwa watengenezaji au kwa waliowauzia ili hatua za uteketezaji ziendelee.

9.            TFDA inaendelea kufuatilia vipodozi vingine vyote ili kujiridhisha na ubora na usalama wake kwa watumiaji. Vile vile itaendelea na kazi yake iliyopewa ya kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba zinazotengenezwa hapa nchini au kuingizwa kutoka nje ya nchi ni bora, salama na zenye ufanisi unaotakiwa. 

10.        TFDA itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na uvunjaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na inawaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo wa bidhaa (chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba) duni au bandia kwenye soko la Tanzania. 


ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOBAINIKA KUWA NA VIAMBATO VILIVYO PIGWA MARUFUKU.

Na.
Jina la kipodozi
Namba ya usajili
Toleo
Tarehe ya kuishamatumizi
Sehemusampuliilipochukuliwa
Aina ya kiambatokilichokutwa
Chemi&Cotex Industries Limited, Dar es Salaam
1.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0095
12&16
Feb-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
2.    
Baby Soft Body Lotion
Haijasajiliwa
08
Dec-16
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
3.    
Siri Moisturizing  Cream- Cocoa Butter
TAN13 CP 3118
26
Jan-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
4.    
Siri Moisturizing  Cream- Lemon
TAN13 CP 3120
03
May- 18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
5.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0094
16
Mar-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
6.    
Lovely Body Cream - Papaya
TAN15 CP0096
10
May-18
Kiwandani
Hydrocortisone
Mamujee Products Limited, Tanga
7.    
Beauty Care Aloe Vera Beauty Cream
Haijasajiliwa
00283
Sep-15
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
8.    
BOSS Hand & Body Lotion
TAN 15 CP 0300
10/0077258
Apr-19
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
9.    
Beauty Care Strawberry Beauty Cream
TAN 13 CP 3559
513
Feb-17
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
10.         
Beauty Care Cucumber Beauty Cream
TAN 13 CP 3694
512
Jul-16
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
11.         
BOSS Hand & Body Cream
TAN 14 CP 4966
10/0077258
Jul-16
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
12.         
Ella Moisturizing Strawberry Hand & Body Lotion
TAN 13 CP 3531
071252
Jun-16
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
13.         
Beauty care – Milk & Honey beauty cream
TAN 13 CP 3413
513, 512
Feb-17
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate& Hydrocortisone
14.         
Stella moisturizing & cleansing cream
TAN 15 CP 0299
10/0077258
Feb-15
Kiwandani
ClobetasolProprionate& Hydrocortisone
15.         
Podoa body cream
TAN 15 CP 0294
006752, 513
Aug-17
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate& Hydrocortisone
16.         
Beauty care – carrot beauty cream
Haijasajiliwa
00277
Aug-17
Kiwandani
ClobetasolProprionate
17.         
Ella Moisturizing carrot Hand & Body Lotion
TAN 13 CP 3695
071252
Dec-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited, Tanga
18.         
Star Rose Lotion
TAN 09 CP 0006
01154
Dec-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
19.         
Goldy Beauty Cream
TAN 14 CP 4890
0539, 0633, 05210
Apr-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
20.         
Skala (Aloe Vera Body Lotion)
TAN 14 CP 4758
02182
Jan-18
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
21.         
Skala Carrot Body cream
TAN 13 CP 3887
1273, 0688
Nov-17
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
22.         
CITIZEN Moisturizing Cream
TAN 09 CP 0391
0294, 0694
Jan-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
23.         
SkalaFor Men Body Lotion
Haijasajiliwa
0454
Mar-18
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
24.         
VESTLINE Body Lotion
TAN 09 CP 0001
10182
Sep-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
25.         
Skala Papaya Body Cream
TAN 13 CP 3888
04106
Mar-18
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
26.         
Baby & Me Baby Cream
TAN 13 CP 3912
01117
Dec-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
27.         
Baby & Me Baby Lotion
TAN 13 CP 3882
0220
Jan-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
28.         
Star Rose Advanced Moisturizing Cream
TAN 14 CP 4691
05169
Apr-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
29.         
Star Rose Advanced Moisturizing Cream
TAN 14 CP 4691
0602
May-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
30.         
Skala Papaya body cream
TAN 13 CP 3888
0662, 0691, 04106
May-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
31.         
Skala aloe vera body cream
TAN 13 CP 3179
0622, 0657
May-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
32.         
Freshia body lotion
TAN 09 CP 0002
03156, 10143
Feb-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate& Hydrocortisone
Tridea Cosmetics Limited, Dar es Salaam
33.         
Cocoa Butter Cream
TAN 11 CP 0717
29, 08
Nov-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
34.         
White Musk Hydrating Lotion
TAN 12 CP 1926
101, 55
Oct-17
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
35.         
Aloe Vera Softy Body Cream
TAN 12 CP 1935
18
Jun-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London, South Africa
36.         
Johnson’s baby lightly fragranced aqueous cream
Haijasajiliwa
0554E25
Mar-17
Kwenye soko
Triamcinolone

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062).
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad