|
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT
Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia) akimtambulisha kwa wananchi mwanachama mpya wa
chama hicho Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Kasulu, mkoani Kigoma Julai 21,2015. Picha na Anthony Kayanda.
Akizungumza baada ya
kukabidhiwa kadi na kiongozi wa ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu
huyo wa NCCR - Mageuzi alisema amejiunga baada ya viongozi wa chama hicho kumhujumu
katika harakati zake za kutetea masilahi ya Halmashauri ya Wilaya Kasulu.
Zitto afichua
Akizungumza katika mkutano huo, Zitto licha
ya kuwataka wananchi wa Kasulu kujiunga na chama hicho, alisema Machali
alishajiunga nao muda mrefu na kwamba alichokuwa anasubiri ni kukabidhiwa kadi.
“Tulisema lazima tupate baadhi ya wabunge na viongozi maarufu kutoka vyama
vingine, sasa tumeanza na Machali na wengine watafuata,” alisema Zitto.
Viongozi wengine waliojiunga na chama hicho
jana ni pamoja na kada wa CCM, Emmanuel Mbwiliza aliyewahi kuwa Diwani wa Kata
ya Nyumbigwa hadi mwaka 2010 pia akiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kuanzia
2007 hadi 2012.
Katika mkutano huo pia viongozi wengine wa
NCCR kutoka Kasulu Mjini na Kasulu Vijijini walijiunga na ACT huku wakiahidi
kupambana kuhakikisha wanashinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Baadhi ya wananchi hao walionyesha kumuunga
mkono Machali katika harakati zake za kutetea Jimbo la Kasulu Mjini kupitia
chama chake kipya wakisema watafanya hivyo kutokana na hulka yake ya kupambana
na viongozi wanaoonekana kufuja mali ya umma.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment