MGOMBEA URAIS UKAWA 2015:-Ifahamu sababu kwa nini Hajatangaza mpaka sasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 22, 2015

MGOMBEA URAIS UKAWA 2015:-Ifahamu sababu kwa nini Hajatangaza mpaka sasa.


Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA.

UKAWA umesema kuwa umeshindwa kumtangaza Mgombea Urais kupitia Umoja huo kutokana na kutopatikana hadi sasa kwa Mgombea Mwenza kutoka Zanzibar.


Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema Bw Tundu Lissu amesema Mgombea Urais kupitia Ukawa ameshapatikana na kwamba kilichochelewesha kutangazwa kwake ni mgombea Mwenza ambaye taratibu za kumpata zinafanyika.

Akihutubia wakazi wa Mji wa Geita, katika viwanja vya Shule ya Msingi Nyankumbu Bw Lissu amesema mgombea wa Ukawa atajulikana hivi karibuni ndani na nje ya nchi.

Amesema umoja huo unaoundwa na Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na NLD utamtangaza mgombea wake mara baada ya kupatikana kwa Mgombea Mwenza.


Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ndiye ambaye anapewa nafasi kubwa ya kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya Ukawa mbele ya mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na kada wa NCCR-Mageuzi, Dk George Kahangwa, lakini hadi sasa vyama hivyo bado vinasita kumtangaza mteule wake.
 
Awali Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Geita, Bw Alphonce Mawazo amesema wakazi wa Geita hawana maeneo ya uchimbaji madini licha ya mkoa huo kuwa na Madini mengi aliyodai kuwa yanawanufaisha wawekezaji.

Source:-Radio Kwizera FM.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad