CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Mechi za Leo July 23, 2015 kwa APR, Al Shandy nao Robo Fainali kesho Yanga SC na KMKM! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 23, 2015

CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Mechi za Leo July 23, 2015 kwa APR, Al Shandy nao Robo Fainali kesho Yanga SC na KMKM!

APR ya Rwanda na Al Shandy ya Sudan Leo July 23,2015 zimemaliza Mechi zao za Kundi B zikiwa nafasi mbili za juu na hivyo kufuzu moja kwa moja kuingia Robo Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, KAGAME CUP 2015.

APR waliichapa LLB AFC ya Burundi Bao 2-1 huku Bao lao la ushindi likifungwa Dakika ya 89 na Bigirimana Issa.

 Katika Mechi hiyo, LLB AFC walitangulia kupata Bao Dakika ya 53 Mfungaji akiwa Nahimana Abdoul Aziz na APR kusawazisha kwa Penati ya Sibomana Patrick katika Dakika ya 58.

Kwenye Mechi ya awali , Al Shandy ya Sudan imeichapa Heegan ya Somalia Bao 3-2 na kutinga Robo Fainali.

Timu za Heegan na LLB AFC sasa zimetolewa rasmi kwenye Mashindano haya kwa vile hawawezi tena kupata hata ile Tiketi ya Mshindi wa 3 Bora kwani Timu za Kundi C, ambazo zimebakisha Mechi, zina Pointi nyingi kuzidi wao na hivyo nafasi ya Mshindi wa 3 Bora itaangukia Kundi hilo.

Kesho Ijumaa, July 24, 2015 ipo mitanange miwili ya Kundi A Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kati ya Al Khartoum na Gor Mahia, kuanzia Saa 8 Mchana na kufuatiwa Saa 10 Jioni Mechi ngumu ya KMKM na Yanga SC.

Mechi hii ni ya mwisho kwa KMKM ambayo itakuwa imecheza Mechi 4 wakati kwa Yanga SC itakuwa ni ya 3 wakibakiza 1 na ikiwa KMKM watafungwa basi wataaga rasmi Mashindano haya lakini wakifungwa Yanga SC bado wanaweza kufuzu wakishinda Mechi yao ya mwisho na Al Khartoum.
RATIBA KAGAME CUP 2015.

Ijumaa Julai 24, 2015

Al Khartoum Vs Gor Mahia [Saa 8 Mchana] 
     
KMKM Vs Yanga [Saa 10 Jioni]

Jumamosi Julai 25, 2015

KCCA Vs Malakia [Saa 8 Mchana]     
 
Adama City Vs Azam [Saa 10 Jioni] 
 
 MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME 2015
 
Kundi A
 

TIMUPWDLGDPTS
1Khartoum220066
2Gor Mahia220036
3Young Africans FC210123
4KMKM3102-23
5Telecom3003-90
Kundi B
 

TIMUPWDLGDPts
1APR330049
2AlShandy311104
3LLB AFC3021-12
4Heegan3012-31
Kundi C
 

TimuPWDLGDPTS
1Azam FC220036
2KCC FC210103
3Malakia2101-13
4Adama City2002-20
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad