RIDHAA URAIS CCM 2015:- Fahamu Kanda ipi inafata baada ya Kanda ya Ziwa kuongoza makada Urais. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 27, 2015

RIDHAA URAIS CCM 2015:- Fahamu Kanda ipi inafata baada ya Kanda ya Ziwa kuongoza makada Urais.

Wakati  vikao vya uteuzi wa kada atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika nafasi ya urais 2015 vikitarajia kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, imebainika kuwa mikoa ya Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kuwa na makada wengi waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa mikoa hiyo ambayo ni Mwanza, Geita, Kagera, Mara, Simiyu na Shinyanga ina makada tisa wa CCM waliochukua fomu kuomba kuteuliwa na chama chao kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015.

 Makada hao ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, Mbunge wa Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere, Mbunge wa Kuteuliwa, Prof. Sospeter Muhongo (Mara) Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (Geita), Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk. Titus Kamani (Simiyu), Balozi wa Urusi, Patrick Chokala, Mbunge wa Sengerema , William Ngeleja ,  Luhaga Mpina (Mwanza), na mtoto wa marehemu Jaji Francis Nyalali, Peter Nyalali (Kagera).

Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ina wagombea saba na Kanda ya Kaskazini inafuatia kwa  kuwa na wagombea sita waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho.

Makada wa CCM waliojitokeza katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof Mark Mwandosya, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, na Musa Mwapango (Mbeya), Mkurugenzi Mstaafu wa Usalama wa Taifa, Hassy Kitine, Dk.  Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Fedha mstaafu, Monica Mbega  (Iringa).

Kanda ya Kaskazini makada wa CCM waliojitosa kuwania urais ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (Arusha), Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha Rose Migiro , Dk.Muzzamil Kalokola,  Litha Ngowi na Hellen Elinawinga (Kilimanjaro), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (Tanga).

Kanda ya Kati inafuatia ikiwa na wagombea watano ambao ni Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangallah (Tabora), Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (Singida), na Dk. Mwele Malecela (Dodoma).

Wagombea kutoka visiwa vya Zanzibar ni Balozi Amina Salum Ali, Makamu wa Rais, Dk.Mohamed Gharib Bilal, Balozi Ali Karume na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustine Ramadhani. 

Aidha, Kanda ya Kusini ina makada wawili ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Lindi).

Kanda ya Magharibi imekuwa ya mwisho kutokana na kuwa na kada mmoja aliyechukua fomu ambaye ni mkulima Lidephonce Bilohe (Kigoma).

Hata hivyo, wapo makada wengine waliojitokeza ambao ni Amos Siyatemi, Samwel John, Leonce Mulenda, Boniface  Ndengo, Maliki Marupu na Veronica Kazimoto.

Hadi kufikia jana June 26,2015, takwimu zinanyesha  makada 40 wameomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti hicho, Vikao vya CCM vitaanza Julai 5, mwaka huu mjini Dodoma na Julai 11,2015 kutafanyika mkutano mkuu kwa ajili ya kuchagua kada mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.

Kanda ya Mashariki ya Pwani inahusisha mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mkoa wa Pwani ambapo hadi sasa hakuna aliyejitokeza. 

ZANZIBAR

Kwa upande wa Zanzibar hadi sasa, makada wa CCM wanaoiomba nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Balozi Amina Salum Ali, Balozi Ali Karume na Jaji Mkuu mstaafu Augustine Ramadhani.

 Makanda wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Amos Robert Siyatemi, Musa Mwapango, Peter Isaiah Nyalali, Leonce Nicholas Mulenda, Boniface Thomas Ndengo na Lidephonce Bilohe.

Chanzo:- NIPASHE

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad