GHASIA BURUNDI:-Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki walaani kupinduliwa Serikali ya Nkurunziza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2015

GHASIA BURUNDI:-Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki walaani kupinduliwa Serikali ya Nkurunziza.

Wakuu wa nchi  za Jumuiya ya Afrika  Mashirika wamelaani jaribio la mapinduzi  yaliyotaka kufanyika nchini Burundi huku wakitaka utawala wa sheria kwa kuheshimu katiba na makubaliano ya arusha pamoja na kusogezwa mbele.

Akisoma maazimio ya mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Jakaya Kikwete amesema wanatambua hali ya kisasa iliyotokea burundi na hivyo wanasisitiza makubaliano ya Arusha yaheshimiwe.

Mkutano huo umekubaliana kwa pamoja uchaguzi wa burundi usogezwe mbele hadi hali ya siasa itakapotengemaa.

Tofauti na matarajio ya wengi Rais Pierre Nkurunziza hakuweza kuhudhuria mkutano huo licha yakuwepo taarifa kuwa aliwasili jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo mkutano huo hakuweza kufanyika katika utaratibu ambao umepangwa kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kuwepo Mapinduzi nchini Burundi ambapo taarifa hizo zimeibua taharuki na wasiwasi miongoni mwa washiriki wa mkutano huo  wakiwemo viongozi kutoka nchi wanachama.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban ki-Moon pichani amewataka wahusika wakuu nchini Burundi kuweka uhasama baina yao kando ilikulinda taifa...BOFYA HAPA KUPATA MUENDELEZO WA KILE KINACHOENDELEA BURUNDI


Rais wa Burundi.

Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare.....Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad