MAAFA:-Watu nane wafa kwa mvua Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 07, 2015

MAAFA:-Watu nane wafa kwa mvua Dar es Salaam.

Watu nane wamekufa na mamia kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zinazonyesha katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau aliyepo jijini Dar es Salaam mvua hizo zimekuwa zikinyesha mfulullizo na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja baadhi ya watu kukosa makazi yao.

Kumekuwa na foleni kubwa ya magari na baadhi ya watu wamechelewa kwenda na kurudi kazini.

Mamlaka ya hali hewa nchini imetahadharisha kuwa mvua hizo zinaweza kuendelea japo zitapungua kidogo.

Aidha Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo kusimama.

Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji  huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa muungano waliopo kata ya goba na  mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo ambapo ITV imeshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa inaninginia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo. 

Wakazi wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi kandokando ya mto mbezi ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto huo zikiendelea kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali kuwapatia viwanja vya bei raisi sehemu nyingine. 

Katika tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha visima vya mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa vyombo vya moto  kukumbwa na adha kubwa ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa mafuta yalichanganyika na maji ya mvua katika kituo cha mafuta  cha kobil kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa madereva hao.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad