VPL 2014/2015:-Cheki Ratiba ya Mechi za wekiendi hii pamoja na Msimamo wa Ligi kuu Tanzania huku Mechi 5 zikibaki. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 17, 2015

VPL 2014/2015:-Cheki Ratiba ya Mechi za wekiendi hii pamoja na Msimamo wa Ligi kuu Tanzania huku Mechi 5 zikibaki.

MSIMAMO VP 2014/2015.

 Wakati Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC wakipeperusha Bendera ya Tanzania kwa kucheza Michuano ya Afrika kwa kuivaa Etoile du Sahel ya Tunisia kwenye Kombe la Shirikisho hapo Jumamosi April 18,2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ligi bila ya wao itaendelea Wikiendi hii kwa Mechi 5.


Ligi itaanza leo Ijumaa April 17, 2015 kwa Mechi moja huko uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kwa Stand United kucheza na JKT Ruvu na  Jumamosi zipo Mechi 3.

Mechi hizo 3 zitachezwa Morogoro kati ya Polisi Moro na Ndanda FC, nyingine ni huko Sokoine, Mbeya wakati Mbeya City watakapoikwaa Simba SC na huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam ni kati ya Azam FC na Kagera Sugar.

Jumapili April 19, 2015 ipo Mechi moja tu huko Mabatini, Mlandizi kwa Wenyeji Ruvu Shooting kuivaa Mgambo JKT.

Yanga SC ndio wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele ya Mabingwa Watetezi Azam FC wanaofuatiwa na Simba SC ambao wako Pointi 4 nyuma ya Azam FC huku Timu zote zikiwa zimecheza Mechi 21 na kubakisha 5.

LIGI KUU VODACOM 2014/2015 -RATIBA

Ijumaa Aprili 17,2015.

Stand United v JKT Ruvu

Jumamosi Aprili 18,2015.

 Polisi Moro v Ndanda FC

Mbeya City v Simba SC

Azam FC v Kagera Sugar

Jumapili Aprili 19,2015.

Ruvu Shooting v Mgambo JKT

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad