UEFA 2014/2015:-Fahamu Matokeo ya Gemu za Jana April 15, 2015 na Ratiba ya Leo PSG v Barcelona na FC Porto v Bayern Munich saa 21.45 Usiku. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 15, 2015

UEFA 2014/2015:-Fahamu Matokeo ya Gemu za Jana April 15, 2015 na Ratiba ya Leo PSG v Barcelona na FC Porto v Bayern Munich saa 21.45 Usiku.


 Estadio Vicente Calderón, Madrid, Spain.

Katika Mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, hii Dabi ya Jiji la Madrrid, hakuna mbabe aliepatikana kati ya Atletico Madrid na Mahasimu wao, Real Madrid, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ulaya baada ya kutoka Sare 0-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA Champions League.

 Timu hizi zitarudiana huko SAntiago Bernabeu Wiki ijjayo.




Juventus Stadium, Turin, Italy

Nao Wenyeji Juventus wameanza vyema baada ya kuichapa AS Monaco Bao 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA Champions League kwa bao hilo la ushindi lilifungwa Dakika ya 57 kwa Penati ya Arturo Vidal iliyotolewa baada ya Beki wa Monaco Ricardo Carvalho kumwangusha Alvaro Morata.

RATIBA ROBO FAINALI UEFA 2014/2015.

Jumatano Aprili 15,2015.

**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu

Paris Saint-Germain v Barcelona

Refa: Marc Clattenburg [England]– Uwanja: Parc des Princes, Paris, France

FC Porto v Bayern Munich 

Refa: Carlos Velasco Carballo [Spain] – Uwanja: Estádio do Dragão, Porto, Portugal
*********************************************************************
UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Robo Fainali-Mechi za Marudiano

**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo

Jumanne Aprili 21,2015.

Bayern Munich v FC Porto [Allianz Arena, Munich, Germany]

Barcelona v Paris Saint-Germain [Nou Camp, Barcelona, Spain]

Jumatano Aprili 22,2015.

Real Madrid v Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain]

AS Monaco v Juventus [Stade Louis II, Monaco, France]

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad