CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga yashinda 2,Jumapili ni Azam FC V/s El Merreikh. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 14, 2015

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga yashinda 2,Jumapili ni Azam FC V/s El Merreikh.

Amisi Tambwe kushoto akifurahia na wapishi wa mabao yake, Mrisho Ngassa kulia na Simon Msuva katikati.

 Yanga SC Leo Februari 14,2015,Majira ya jioni ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam imeichapa Klabu ya Botswana BDF XI Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.

Bao zote za Yanga SC zilifungwa na Straika wao Amisi Tambwe anaetoka Burundi moja katika kila Kipindi.

Tambwe alifunga Bao la Kwanza Dakika ya Kwanza tu ya Mchezo alipounganisha kwa Kichwa Krosi ya Simon Msuva na kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 55 pia kwa Kichwa baada ya Krosi safi ya Mrisho Ngassa.

Timu hizi zitarudiana huko Botswana Wiki mbili baadae na Mshindi wake atatinga Raundi ya Kwanza kucheza na Mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na FC Platinum ya Zimbabwe.
Hapo Kesho Februari 15,2015 Jumapili, Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watakuwa kwao Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuivaa El Merreikh ya Sudan katika Mechi ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Timu nyingine mbili za Tanzania ambazo pia zimo michuano ya CAF Barani Afrika ni KMKM na Polisi, zote za toka Zanzibar, ambapo  Wikiendi hii zinaanzia Ugenini kwa KMKM kucheza Sudan na Al Hilal kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI  na Polisi kucheza Nchini Gabon na CF Mounana kwenye Kombe la Shirikisho.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad