|
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (walio kaa mwenye miwani) akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kufungua Mkutano huo, Januari 08,2015, mjini
Dodoma.
(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa Serikali inatarajia
mwezi Februari mwaka huu kuanza uandikishaji na uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric
Voter Registration (BVR) ili kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura ambapo
maboresho hayo yatafuta matumizi ya vitambulisho vya kupigia kura vya sasa.
Turuka
alifafanua kuwa maboresho ya daftari hilo nchini yatafanyika kwa watu wote
wenye sifa za kupiga kura Oktoba mwaka huu na kukamilika kabla ya kura ya maoni
ya Katiba, katika kura ya maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa 2015,
mpigakura atatumia kitambulisho kipya atakachopatiwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), baada ya kuandikishwa upya katika mfumo huo.
Akiongea
mara baada ya kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo, mjini
Dodoma, Turuka alibainisha kuwa tayari serikali imefanikiwa kuifanyia
majaribio teknolojia hiyo ya BVR katika majimbo matatu ya hapa nchini ambayo
ni; Jimbo la Kawe – Dar es Salaam , Jimbo la Kilombero - Morogoro na
Mlele - .
“Serikali
imefanikiwa kutekeleza kwa ufanisi jaribio la teknolojia ya BVR japo
ambapo changamoto zilizo jitokeza katika majaribio hayo tayario
tumeshazifanyia kazi katika kuboesha zoezi hilo, hivyo napenda kuwatoa hofu
wananchi kuwa teknolojia hiyo ya kisasa kuwa lengo la serikali la kutumia
teknolojia hiyo ni kumuwezesha mwananchi kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia
njia ya kisasa hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi wakati zoezi hilo
litakapo anza kwani tunaandikisha wapigakura ” alisistiza
Turuka
BVR ni mfumo wa kuchukua taarifa za mtu za kibaiolojia hasa alama za vidolya e
kwa ajili ya kuzihifadhi katika kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi.
Mwaka 2004, NEC ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni pamoja na
ukusanyaji wa taarifa za wapigakura na uhifadhi wa taarifa za kielektroniki.
Wapiga kura wa zamani kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa watatakiwa
kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa za vidole,
picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho
vipya .
|
No comments:
Post a Comment