TAARIFA KWA VYOMBOVYA HABARI.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,(Pichani)
amefanyauteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekitina Makamishna wanne wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Borakama ifuatavyo:-
Mwenyekiti:
Bwana Bahame
Tom Mukirya -NYANDUGA: Ana Shahada ya Sheria, 1977 (Dar es Salaam), Shahada ya
Uzamili ya Sheria, 1987, (London) na Diploma ya Uzamili ya Sheria, 1981 (The
Hague). Alifanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa wa Kimataifa kwa
miaka 17.
Alikuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea wa Tanganyika,
2001-2009.
Alikuwa Kamishna wa Umoja wa Afrika wa Kamisheni ya Haki za Binadamu
(2003-2009). Ni Mtaalam Huru wa Somalia wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki
za Binadamu, (2014).
Makamu
Mwenyekiti:
Bwana Iddi
Ramadhani MAPURI - Ana Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1984 na Diploma
ya Uzamili ya Maendeleo Vijijini, 1987 na Diploma ya Uzamili ya Menejimenti
(India). Alikuwa Kamishna wa Kazi, 1989-2010.
Ni Mkurugenzi wa Utawala na
Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Wizara ya Vijana, Wanawake na Uwezeshaji
tangu 2011.
Makamishna:
1. Bwana
Mohamed Khamis HAMAD - Ana Shahada ya Sheria, 2004 (Zanzibar), na Shahada ya
Uzamili ya Sheria 2007 (Oslo). Ni Wakili wa Serikali Mwandamizi katika Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka. Alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Rufani za Kodi.
Alikuwa pia Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Tume ya Kurekebisha Sheria.
2. Dkt.
Kevin MANDOPI - Ana Shahada ya Sheria, 2003 (Dar es Salaam), Shahada ya Uzamili
ya Sheria, 2007 (Dar es Salaam) na Shahada ya Uzamivu, 2013 (St. Augustine
University), Mwanza. Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria, Chuo
cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto. Ni Wakili wa Kujitegemea tangu 2005. Ni
Mhadhiri wa Sheria.
3. Bibi
Rehema Msabila Ntimizi-Ana Shahada ya Sheria, 2001 (Dar es Salaam) na Shahada
ya Uzamili ya Sheria, 2003 (Dar es Salaam). Alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali
2005-2007; Kaimu Msaidizi Mwandamizi wa Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi,
1994-2005. Ni Meneja wa Ulinzi wa Mali Vijijini, MKURABITA, (tangu 2008).
4. Bibi
Salma Ali HASSAN -Ana Shahada ya Sheria, 2001 (Malaysia) na Shahada ya Uzamili
ya Menejimenti, 2009 (Malaysia). Alikuwa Wakili wa Serikali, 2002-2009, Afisa
wa Haki za Binadamu, Wizara ya Katiba na Utawala Bora. Ni Wakili wa Kujitegemea
tangu 2011.
Uteuzi huo
unaanzia tarehe 06 Januari, 2015, na wataapishwaIkulu, Dar es Salaam siku ya
Alhamisi,tarehe 8 Januari 2015, saa sita adhuhuri.Imetolewana;Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,Ikulu – Dar es Salaam.07 Januari, 2015
|
No comments:
Post a Comment