SOMA HII:-Ni kuhsu ''Panya Road'' ni vikundi vidogo vidogo vya watoto wahuni …. wakamatwa kwa Uhalifu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 05, 2015

SOMA HII:-Ni kuhsu ''Panya Road'' ni vikundi vidogo vidogo vya watoto wahuni …. wakamatwa kwa Uhalifu.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia baadhi ya vijana wanaotuhumiwa kufanya vurugu kwa kuwapora watu mali.

Kundi la kihuni la vijana linalojulikana kama ''Panya Road'' lilifanya vurugu kwa kuwapora watu mali zao na kwenye maduka ya mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini , Advera Bulimba amesema vijana 36 walikamatwa na wanahojiwa.

Amefahamisha kuwa vijana hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika.

Aidha Msemaji wa Jeshi la Polisi amefafanua kuwa ''Panya Road'' ni vikundi vidogo vidogo vya watoto wahuni wanaojiingiza katika vitendo vya uhalifu.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad