MAPINDUZI CUP 2015:- Nusu Fainali Januari 10,2015 baada ya Yanga SC na Azam FC kutupwa Nje.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 09, 2015

MAPINDUZI CUP 2015:- Nusu Fainali Januari 10,2015 baada ya Yanga SC na Azam FC kutupwa Nje.!

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman akikabiliana na beki wa JKU usiku Uwanja wa Amaan .

Wana Jangwani Yanga SC wanapanda boti moja na Azam FC leo Januari 09,2015, kurejea Jijini Dar es Salaam kufuatia kutolewa katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2015 na timu ya JKU kwa kufungwa bao 1-0 usiku wa jana Januari 08,2015,kwenye mechezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Shukaa wa JKU, alikuwa ni mshambuliaji Amour Omar ‘Janja’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 72 kwa shuti kali lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, akiwa chini akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi katika mchezo wa Robo fainali ya Kombe la Mapinduzi 2015.

JKU ilitawala sehemu ya kiungo katika mchezo wa huo na Yanga SC ilipitisha mashambulizi mengi kupitia kwa mawinga hatari, Simon Msuva na Andrey Coutinho, lakini washambuliaji Amisi Tambwe na Kpah Sherman walishindwa kufunga. 

JKU sasa watacheza Nusu Fainali hapo Jumamosi Januari 10,2015 na Mtibwa Sugar ambao mapema jana Januari 08,2015 waliibwagwa Azam FC kwa Penati 7-6 baada ya Mechi yao ya kumalizika 1-1.

Nusu Fainali nyingine itakayochezwa Siku hiyo hiyo Jumamosi ni kati ya Polisi ya Zanzibar na Simba SC.

Polisi waliwavua Ubingwa KCCA ya Uganda baada ya kutoka nao Sare 0-0 na hatimae kushinda kwa Mikwaju ya Penati 5-4 mapema na Simba kuitwanga Taifa ya Jang’ombe 4-0 .

  UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad