MAPINDUZI CUP 2015:-Nusu fainali Januari 10,2015 –Simba SC Vs Polisi,Mtibwa Vs Yanga au JKU. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 08, 2015

MAPINDUZI CUP 2015:-Nusu fainali Januari 10,2015 –Simba SC Vs Polisi,Mtibwa Vs Yanga au JKU.

Kikosi cha Polisi Zanzibar (Pichani) kimekuwa cha kwanza kwa timu za visiwani kusonga hadi Nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2015.

Polisi imefanikiwa kutinga nusu fainali kwa kuishinda Bingwa mtetezi KCCA ya Uganda kwa mikwaju ya penalti 6-5 leo Januari 08,2015,Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, timu hizo zilimaliza kwa sare ya bila bao dakika 90 na kulazimisha changamoto ya mikwaju ya penalti kuchukua nafasi.
Simba SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali, jana Januari 07,2015,baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0.

Alikuwa ni IBRAHIM AJIBU, Mchezaji aliekuzwa toka Simba B, alipiga Hetitriki na kuipeleka Simba Nusu Fainali ya Mashindano ya Mapinduzi Cup 2015.

Bao jingine la Simba lilifungwa na Shaaban Kisiga.

Leo Januari 08,2015,zipo Mechi 3 za Robo Fainali zitakazoanza kwa Mechi kati ya KCCA v Polisi na kufuatia Azam FC v Mtibwa Sugar na kumalizia kwa Yanga kuivaa JKU.

Washindi wa Mechi hizi watatinga Nusu Fainali.

Robo Fainali Januari 07,2014

2015 Yanga v JKU [RF4]

Jumamosi Januari 10,2015

Nusu Fainali

Simba v  Polisi

 Mtibwa Sugar v Yanga au JKU

Jumanne Januari 13,2015.

Fainali

Nayo timu  ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Januari 08,2015, imetinga fainali za Kombe la Mapinduzi kwenye michuano hiyo inayoendelea Visiwani Unguja katika mchezo uliomalizika usiku huu.

Katika mchezo huo Mtibwa ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ally Shomari katika dakika ya 63 akimalizia pasi ya Mussa Hassan Mgosi ndani ya eneo la hatari.

Bao la kusawazisha la Azam Fc lilifungwa na Herman Kipre Tchetche katika dakika ya 89, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Himid Mao, na kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zikimalizika matokeo yalikuwa ni 1-1 na kufikia hatua na kupigiana penati (Matuta).

Katika penati tano za kwanza timu zote zilikosa  penati moja moja, ambapo kwa upande wa Mtibwa Sugar, aliyekosa alikuwa ni Amme Ally na kwa upande wa Azam Fc, aliyekosa alikuwa ni Kipre Tchetche.
  
Na Penati ya mwisho iliyowaondosha Azam ilikwa ni ya Aish Manura, iliyopanguliwa na kipa wa Mtibwa Sugar.
 UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad