LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Manchester United yaanza mwaka 2015 kwa sare 1-1. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Thursday, January 01, 2015

demo-image

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Manchester United yaanza mwaka 2015 kwa sare 1-1.

.com/simgad/
falcaoooooo

Radamel Falcao akiutazama mpira wake ukitinga kwneye wavu wa Stoke City huku kipa Asmir Begovic akiruka bila mafanikio.

 Mechi ya kwanza kabisa kwa Mwaka Mpya 2015 ,Ligi kuu soka Nchini Uingereza huko Britannia Stadium ilimalizika kwa Sare ya 1-1 kati ya Wenyeji Stoke City na Man United.

Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1 licha ya Man United kutawala.Wenyeji Stoke City ndio waliotangulia kufunga baada ya Dakika 2 tu baada ya Kona yao kuunganishwa kwa Kichwa na Peter Crouch na Mchezaji wa zamani wa Man United Ryan Shawcross kuutumbukiza Mpira wavuni.

falcaoooo

falcao

ryna-shwa

shawcross

Kipa wa United David De Gea na mabeki wake wakiuangalia mpira wa Ryan Shawcross ukielekea wavuni .

Man United walisawazisha katika Dakika ya 26 kufuatia Kona ya Nahodha Wayne Rooney kuparazwa kwa Kichwa na Michael Carrick na Radamel Falcao  kuunganisha Mpira wavuni.

Kipindi cha Pili hakikuzaa Bao zozote licha ya nafasi kadhaa hasa kwa Stoke ambao Straika wao Peter Crouch alipiga Kichwa na kugonga mwamba na kuokolewa....Matokeo haya yameibakisha Man United Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 37.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *