|
Picha ikionyesha mabaki ya ndege ya AirAsia kutoka
baharini.
MKIA wa
Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea na watu 162, Desemba 28, mwaka jana
2014,umepatikana leo Januari 07,2015, katika Bahari ya Java, Indonesia.
Eneo la mkia
ndipo kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege 'black box' kinapatikana na
upatakianaji wake utasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ndege hiyo kupotea na
kisha kuanguka baharini.
Ndege hiyo
ilikuwa ikitokea Jiji la Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singaporea. Mpaka
sasa miili 40 imeopolewa kutoka baharini katika eneo ambalo ndege hiyo
ilianguka.
|
No comments:
Post a Comment