![]() |
|
Kuna watu uhusiano wao unawaka moto kwa migogoro ya kila
siku. Wengine ni marafiki kwa maana ya wapenzi lakini pia kuna wanandoa ambao
nyumba zao zinayumba.
Wanatumia muda mwingi kuzungumzia migogoro badala ya
mambo mengine ya msingi katika ndoa yao.
Kuungana katika ndoa kunamaanisha
kusaidiana. Mwanamke anakwenda kuwa msaidizi wa mwanaume wake.
Kukikosekana amani maana yake kila mmoja atakuwa kivyake;
kama ndivyo, maendeleo kwenye familia yatatokea wapi?
Ndugu zangu, WANAWAKE NDIYO MSINGI WA MAFANIKIO KATIKA
NDOA.
Hata kama baba anatafuta kiasi gani kama hatakuwa na mwanamke ambaye
anampa amani, ni wazi kwamba fedha anazosaka zitapotea!
Hapa nitakupa siri muhimu ambazo wanawake wengi hawazijui
kuhusu wanaume.
Heshima, unyenyekevu.
Mwanaume
kiasili ni kiongozi wa mwanamke, hivyo ikiwa mwanamke wake ataonyesha
hakubaliani na uongozi wake, akashindwa kumnyenyekea kwa mapenzi mazito, ni
wazi atapoteza nafasi yake au hata kama itaendelea kuwepo haitakuwa na nguvu.
Uanaume.
Mwanaume anajiamini lakini anajisikia
vizuri kama mwanamke wake atatambua, kuthamini na kuonyesha uhitaji wa uanaume
wake. Siku zote anapenda aonekane ndiye mwamuzi wa mambo magumu. Mshauri mkuu
na kiongozi bora.
Jaribu kuwa karibu na mwanaume wako, mshirikishe katika
mambo na onyesha wazi kuwa bila yeye, huwezi kukamilisha jambo lako. Huu ni
uchawi mkubwa sana kwa wanaume.
Kubanwa.
Wanaume wengi hawapendi kufuatiliwa
sana, hawapendi kubanwa na kuulizwa kila mara mahali walipo (hasa baada ya muda
wa kazi).
Kumbana humaanisha humwamini au hutaki kumpa nafasi angalau ya
kukutana na rafiki zake.
Ukimpa uhuru utashangaa anaongeza mapenzi na atakuja na
mambo mengi mapya ambayo si ajabu atakuwa amejifunza kutoka kwa wenzake.
Mahaba ya wazi.
Ni kweli kwamba kuonyeshana
mapenzi ya wazi hunogesha penzi lakini kwa wanaume ni tofauti kidogo.
Mfano,
mwanamke hujisikia fahari zaidi, akishikwa mkono na mwanaume wake na kuongozana
kwenye hadhara lakini wanaume wengi hawana hulka hiyo.
Ni muhimu kuchunguza,
je, mwenzako anapenda? Maana yawezekana kati ya wachache wanaopenda, mwanaume
wako yupo.
Kuitikia hisia.
Unatakiwa kumjua mwanaume wako
na kuitikia hisia zake. Msome na umjue. Mpe anachohitaji kwa wakati uleule
anaotaka.
Hiyo itakufanya uwe mwanamke sahihi kwake na siyo mzigo!
UNGANANASI
KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Wednesday, December 17, 2014
UHUSIANO:- Siri usizozijua kuhusu Wanaume..’’
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment