|
NGARA.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Cornel Ngudungi amebatilisha
matokeo ya uchaguzi katika vitongoji vya Mnyange na Mukasasa kwenye kijiji cha
Murukulazo na kuagiza uchaguzi urudiwe kesho baada ya kujitokeza dosari kadhaa ikiwemo
idadi ya kura kuzidi ile ya waliopiga kura
Bw Ngudugi
ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo amesema hayo leo kufuatia wagombea
wa Chadema na CCM kugoma kusaini fomu ya matokeo baada ya kubaini kuongezeka
kwa idadi ya kura tofauti na idadi ya wapiga kura waliojiandisha katika kituo
hicho
Amesema
kitendo cha kuongezeka kwa idadi ya kura tofauti na idadi ya walioandikishwa ni
kosa kubwa hivyo uchaguzi unapaswa urudiwe baada ya kushauriana na viongozi wa
vyama vya siasa na kamati ya ulinzi na usalama
Diwani wa
kata ya Murukulazo Bw Mkiza Byamungu amesema kura 9 zimeongezeka katika kituo
cha Mukasasa na kwamba katika kitongoji cha Mnyange walikoshinda CCM ambapo
baadhi ya wapiga kura wamezuiwa kupiga kura baada ya majina yao kuwekewa alama
kuwa tayari wamepiga kura
KIBONDO.
Chama cha
Mapinduzi, CCM Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kimeongoza katika uchaguzi wa
Serikali za mitaa kwa kupata viti 34 vya Wenyeviti wa vijiji kati ya nafasi 50
zilizoshindaniwa sawa na asilimia 76
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo msimamizi Mkuu wa uchaguzi Wilayani Kibondo Bw
Judethadius Mboya amesema Chadema wamepata viti 9 sawa na asilimia 12, NCCR
Mageuzi viti vitano sawa na asilimia 9 huku Chama cha Wananchi CUF kikipata
viti viwili sawa na asilimia 1.4
Amesema katika
nafasi ya vitongoji CCM imepata viti 284, Chadema viti 47, NCCR Mageuzi
wamepata viti 33 huku Chama cha Wananchi CUF kikipata viti vitano
Bw Mboya
amesema wilaya ya Kibondo imefanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua
Wenyeviti wa vijiji 50, Wenyeviti wa vitongoji 369 na wajumbe wa serikali za
vijiji 700
MWANZA.
Halmashauri
ya wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza imekamilisha zoezi la kuchambua matokeo ya
uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ngazi ya vijiji, ambapo Chama cha Demokrasia
na Maendeleo kimeongoza
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bw Octavian Mapunda amesema Chadema
kimeshinda katika vijiji 47 kati ya vijiji 76
Amesema
Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda kwenye vijiji 27 huku Chama cha Wananchi CUF
kikishinda kwenye kijiji kimoja pekee
Amesema
zoezi la kuchambua matokeo ya ngazi ya vitongoji bado linaendelea ambapo
amewaomba wananchi kuwa watulivu ili kutoa muda wa kutosha kukamilisha kazi
hiyo
Bw Mapunda
amesema wilaya hiyo ina jumla ya vitongoji 512 ambapo kati ya hivyo vitongoji
vinne havikufanya uchaguzi na kwamba vitarudia uchaguzi huo.
SINGIDA.
Chama cha
Mapinduzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kimepata ushindi wa wastani
wa asilimia 95 katika uchaguzi wa serikali za Mitaa
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Singida Bw Joseph Mchina ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi
katika eneo hilo amesema zoezi la upigaji kura, kuhesabu hadi kutangaza matokeo
limefanyika kwa amani na utulivu
Akitangaza
matokeo hayo Bw Mchina amesema kati ya Mitaa 50 iliyopo katika Manispaa hiyo,
Chama cha Mapinduzi kimepata ushindi wa asilimia mia moja baada ya kushinda
viti vyote na kuwabwaga wapinzani wake wa CUF, Chadema na ACT
Bw Mchina
amesema kati ya vijiji 20 vilivyopo, CCM imeshinda vijiji 19 sawa na asilimia
95 wakati chama cha wananchi CUF kimepata kiti kimoja kwa nafasi ya Uenyekiti
Kwa upande
wa vitongoji, CCM imepata ushindi wa asilimia 90, CUF asilimia 8.9 wakati
Chadema kimeshinda kwa asilimia 1.1
Chanzo:-Radio
Kwizera FM-Ngara/Harakati News.
|
No comments:
Post a Comment