|
Kutokana na meli ya Mv Victoria kukwama safari zake mara kwa mara na
kuzua mjadala na hasara kwa abiria na wafanyabiashara, waziri wa uchukuzi
KHARISON MWAKYEMBE atimua uongozi mzima bandarini hapo na kuteua wapya..Picha/Habari na :-Harakati News.
Waliofukuzwa kazi ni Meneja mkuu Projest Kaija, na nafasi yake
imechukuliwa na Fabian Mayenga.
Kaimu mhasibu mkuu Tito W.Mwambagi, nafasi yake kuchukuliwa na Beatus R.
Rugalabamu, kaimu meneja masoko biashara, ameondolewa Cpt Obeid Nkongoki nafasi
yake inachukuliwa na Cpt Winton Mwasa.
Aliyefukuzwa mwingine ni kaimu meneja wa tawi Mwanza Beatus T. Mghamba na
kuingia Bwana Philemoni Bagambilana, Kaimu tawi Kigoma ameondolewa Bwana Abel
Giliard na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Stephen, huku kaimu mwanasheria
na menejautumishi anakuwa Fabian Mayenga baada ya kuondolewa Josephat Mshumbusi
.
Meli hiyo imesimamishwa kutoa huduma ili ifanyiwe ukarabati wa kina,
baada ya kubainika kuwa uongozi uliokuwapo ulikuwa ukiweka spare fake, na
kusababisha adha kubwa kwa watumiaji
Uongozi mpya umeanza kazi tangu tarehe 18 Dec 2014.
|
No comments:
Post a Comment