MAJANGA:- Ngumi zapigwa Bungeni nchini Kenya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 18, 2014

MAJANGA:- Ngumi zapigwa Bungeni nchini Kenya.

Seneta Johnston Muthama aliyejeruhiwa mguuni na kuchaniwa suruali yake wakati wa vurugu bungeni leo Desemba 18,2014.

Wabunge nchini Kenya leo Desemba 18,2014, wametofautiana bungeni na kuamua kutupiana makonde huku wengine wakichaniana nguo kufuatia mjadala kuhusu muswada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa Wakenya.
Bunge nchini Kenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 kufuatia mtafaruku huo.
Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha muswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais Kenyatta kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani waliupinga muswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kutaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa muswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa muswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa Bunge hilo, Justin Muturi kuna kipindi alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjadala ambao ulitarajiwa kuwaka moto, hasa wa upande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bungeni kufuatia matukio ya ukosefu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwa wa ugaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.

Mapendekezo ya muswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.

Pia ikiwa muswada huo utapitishwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadi shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Muswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wanaowataka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia.

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kuimarisha usalama wa tangu mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad