LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Mbwembwe za Simba zaishia kwa Kagera Sugar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 27, 2014

LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Mbwembwe za Simba zaishia kwa Kagera Sugar.

Wekundu wa Msimbazi wameendelea kuchechemea katika ligi kuu Soka Tanzania bara 2014/2015 baada ya jana Desemba 26,2014  kulala kwa bao moja kwa bila uwanja wa taifa. 

Simba SC imepoteza mechi ya kwanza kwenye ligi hiyo baada ya kutoka sare sita na kushinda mechi moja katika mechi saba zilizopita.

Huku ikitarajia kupata ushindi wa pili baada ya kurekebisha kikosi chake kwa kufanya usajili wa baadhi ya wachezaji na kuifunga Yanga mabao 2-0 kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe2, Simba SC ilijikuta ikishindwa kufurukuta nyumbani.

Kagera ilipata bao lake latika dakika ya 10 ya mchezo likifungwa na Atupele Green kwa kichwa baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Simba, Ivo Mapunda.

Matokeo hayo yameifanya Kagera Sugar kusogea kwenye msimamo mpaka nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 13, Simba SC ikibaki nafasi ya nane na pointi zake tisa.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad