HEKINA NA BUSARA:-Rais JK akatisha ziara ya Pinda Uarabuni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 18, 2014

HEKINA NA BUSARA:-Rais JK akatisha ziara ya Pinda Uarabuni.

Rais wa Tanzania,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete .

 Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Waziri mkuu wa Tanzania Bw.Mizengo Pinda.

Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Desemba 18,2014,Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.

Baadaye leo Desemba 18,2014,Waziri Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23,2014.

Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.



UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad