EPL 2014/2015:-Taswira ya Liverpool v Arsenal walivyotoshana Nguvu mechi ya Ligi kuu Desemba 21,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 22, 2014

EPL 2014/2015:-Taswira ya Liverpool v Arsenal walivyotoshana Nguvu mechi ya Ligi kuu Desemba 21,2014.

Sterling receives the Tuttosport European Golden Boy award for 2014 before the Barclays Premier League match at Anfield.

A Liverpool fan backing manager Rodgers with a sign reading: 'Brendan, I've got your back' ahead of kick-off on Sunday afternoon

Liverpool hapo jana Desemba 21,2014 majira ya usiku, wakicheza kwao Anfield, wamejinusuru kufungwa na Arsenal  kwa kusawazisha Bao katika Dakika ya 96 walipotoka nyuma kwa Bao 2-1 walipocheza na Arsenal na Refa Michael Oliver kuongeza Dakika 9 za nyongeza kufidia muda ambao Beki wao Martin Skrtel alipokuwa akitibiwa na ni yeye Skrtel ndie alisawazisha Bao hilo kwa Kichwa.

Liverpool walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 45 kupitia Phillippe Coutinho na Arsenal kusawazisha Dakika moja baadae kwa Bao la Mathieu Debuchy.

Kipindi cha Pili, Olivier Giroud aliipa Arsenal Bao la Pili na lilidumu hadi Dakika ya 90 ambapo Refa Michael Oliver aliongeza Dakika 9 za Majeruhi na Dakika 3 baadae Liverpool kubaki Mtu 10 baada ya Fabio Borini kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kumchezea Rafu Cazorla.

Zikiwa zimebaki Dakika 3 za muda wa Majeruhi uliongezwa kwa kuumia Sentahafu wa Liverpool Martin Skrtel, Beki huyo huyo ndie alieunganisha Kona ya Adam Lallana kwa Kichwa na kuipa Liverpool Sare ya Bao 2-2.



Matokeo haya yamewaacha Liverpool wakiwa Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 22 huku Arsenal wakiwa Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 27 na Timu zote zikibaki kutupwa mbali kidogo na Timu 4 za juu ambapo Timu iliyo Nafasi ya 4, West Ham, ina Pointi 31.

Ligi Kuu England itaendelea Jumatatu Usiku wakati Vinara wa Ligi Chelsea watakapotembelea Britannia Stadium kucheza na Timu ngangari Stoke City.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad