Taarifa
muhimu kabla ya kutumia ampicillin:
Baada ya
kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa una U.T.I unatakiwa kujadiliana na daktari
kuhusu dawa atakazokupatia. Kuwa huru na muwazi kumweleza daktari kuhusu
mstakabali wa afya yako.
Mweleze
daktari au mfamsia au muuguzi kama una ujauzizo au unapanga kupata ujauzito
wakati ukitumia ampicilini au unanyonyesha.
Baadhi ya dawa katika kundi la
vijiuasumu haziruhusiwi kwa kuwa zinaweza kuwa na madhara kwa mtoto aliyeko
tumboni.
Hata hivyo ampicillin inaweza kutumia. Kumbuka kutokutomia dawa pasipo
maelekezo ya daktari hasa wakati wa ujamzito au kunyonyesha. Pia mweleze
daktari, mfamasia au muuguzi kama unatumia dawa nyingine za tiba au vyakula
nyongeza (food supplement), huwa unapata mzio ukitumia baadhi ya dawa au
vyakula na una matatizo ya tumbo au kuharisha. Taarifa hizi zitakusaidia wewe
kuandikiwa dawa zitakazokufaa kulingana na hali yako ya kiafya.
Baadhi ya
dawa za tiba haziwezi kufanya kazi sanjari na dawa nyingine. Ampicillin pia
zina tabia hii.
Mweleze daktari kama unatumia dawa yoyote kabla hajakuandikia
dawa. Baadhi ya dawa ambazo hazitumiwi sanjari na ampicillini ni tetracycline
hasa doxycline. Dawa hii huingilia utendaji kazi wa ampicillin mwilini na
kuifanya kukosa ufanisi.
Dawa nyingine ambazo hazipaswi kutumika sambamba na
ampicillin ni Probenecid, Allopurinol, Anticoagulants (heparin, warfarin) au
methotrexate na Aminoglycosides (mfano; gentamicin. Probenecid huongeza madhara
kwa mgonjwa kama tutakavyoona baadaye na Allopurinol inaweza kuongeza vipele
kwenye mwili.
Kwa upande
wa Anticoagulants hasa heparin, warfarin au methotrexate, haishauriwi kwa kuwa
ampicillin inaweza kumwongezea madhara mgonjwa. Haya ni madhara ambayo kila
anayetumia dawa huyapata na yanavumilika.
Dawa za
Aminoglycosides hasa gentamicin na za kupanga uzazi hazitumiki sanjari na
ampicillin kwa kuwa zinaweza kupunguzwa nguvu ya utendaji kazi wake mwilini.
Zinaweza
kuwepo dawa nyingine zisizopaswa kutumika sanjari na ampicillin, unachoshauriwa
kufanya ni kumweleza daktari kama unatumia dawa nyingine za tiba.
MATUMIZI
SAHIHI YA DAWA
Tumia
ampicillin kama ulivyoelekezwa na daktari. Itumie kwa kiasi, muda na wakati,
kadri ulivyoelekezwa na daktari. Usiongeze wala kupunguza kiasi cha dawa na
muda wa kuzitumia, ili kuepusha madhara. Maelezo juu ya kifungashio cha dawa
hii yatakusaidia kutumia ampicillin kwa usahihi.
Tumia ampicillin
kwa kunywa angalau nusu saa kabla ya kula au saa mbili baada ya kula. Kunywa
maji ya kutosha, kadri daktari atakavyokuelekeza, wakati unatumia dawa hii.
Ili uweze
kupata nafuu au kupona kabisa tumia dozi nzima ya ampicillin. Usikatishe dozi
hata kama utajisikia kupona.
Ikitokea
umesahau kutumia dawa, tumia mara moja mara baada ya kukumbuka. Kama umekumbuka
wakati wa kutumia dawa umekaribia, usitumie dawa, subiri dozi inayofuata na
kisha urejee katika utaratibu wako wa awali.
TAHADHARI
Usiitumie
kutibu magonjwa yanayoambukizwa na virusi kama vile baridi.
Imeandaliwa
na Martin Malima kwa msaada wa mitandao.
|
No comments:
Post a Comment