SOKA WILAYA YA NGARA:-Taswira ya Utata wa goli wakati Walimu FC wakifuzu Nusu Fainali kwa Kishindo cha goli 8-6. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 19, 2014

SOKA WILAYA YA NGARA:-Taswira ya Utata wa goli wakati Walimu FC wakifuzu Nusu Fainali kwa Kishindo cha goli 8-6.

Pamoja na mchezo kusimama dakika kadhaa kufuatia utata wa uliofanywa na Mwamuzi msaidizi kukubali goli ambalo halikuingia wavuni,Timu ya soka ya Walimu FC imekata tiketi ya kucheza  Nusu Fainali ya Ligi soka  wilaya ya Ngara mkoani Kagera yenye lengo ya kupata Bingwa wa wilaya 2014/2015,baada ya jana October 18,2014  jioni,kuifunga timu ya Benaco Stars kwa jumla ya mabao 8-6. 

Mchezo huo wa hatua ya robo fainali uliochezwa uwanja wa Kokoto mjini Ngara,ilizishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 90 kwa kufungana bao 3-3 na ndipo zikaongezwa dakika 30 ambazo ziliwapa Walimu FC ushindi kupitia Matuta baada ya kupata penati zote 5 huku Benaco Stars wakikosa moja na kupata 3.

Mashabiki wakielezea kwa wasimamizi wa Ligi hiyo,Chama cha soka wilaya -NDFA kuwa goli lililokubaliwa na Mshika Kibendera namba moja kuwa si goli kwani limepita nje ya goli.

Kufuatia utata huo ulisababisha jazba kwa Wachezaji wa Walimu FC hali iliyotaka kuwafanya wagomee mchezo ,lakini Busara ya Viongozi wao na Wale wa chama cha Soka NDFA  ukawafanya kurejea uwanjani kuendelea na mchezo na hatimaye kufuzu nusu fainali kwa Penati 8-6.

Jumapili October 19,2014 ,Ngara Boys watakuwa wenyeji wa Rulenge White Stars saa 10 jioni Katika uwanja huo wa Kokoto.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad