PIGO BONGO MUVI:- Mzee Manento amefariki dunia Jana October 29,2014 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 30, 2014

PIGO BONGO MUVI:- Mzee Manento amefariki dunia Jana October 29,2014

Mzee Manento enzi za uhai wake.

Msanii wa filamu za Kibongo, Mzee Manento amefariki dunia jana October 29,2014,  jioni akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mzee Manento alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mzee Manento atakumbukwa katika filamu alizocheza kama 'Hero of the Church', 'Dar to Lagos', 'Fake Pastor' na nyinginezo. 

Ndugu, jamaa na marafiki kwa sasa wamekutana nyumbani kwa marehemu huko Kigogo, Dar es Salaam kujadiliana kuhusu taratibu za mazishi.

Aidha msiba huu unakuja ikiwa ni Wiki moja  baada ya kutokea kwa msiba wa mmoja wa wasanii wa TMK Wanaume Family YP na saa chache baadaye ukatokea msiba mwingine wa aliyekuwa msanii wa maigizo na vichekesho Sherry Mwana. 

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEEN!

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad