|
Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) lawawezesha vijana Mkoani Kagera kujiajili kwa kuwapatia
mashine 32 za kisasa za kufyatua matofali yenye gharama nafuu zenye jumla ya
gharama ya shilingi 14,400,000/=.
Mashine hizo
zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe ofisini
kwake kwenye hafla fupi na mwakilishi wa shirika la Nyumba la Taifa Bw.Adrian Dominick September 01, 2014.
|
|
Katika hafla
hiyo Mkuu wa mkoa alizikabidhi mashine hizo kwa Wakurugenzi na Wenyeviti wa
Halmashauri nane za Mkoa wa Kagera kwajili ya kuzikabidhi mashine hizo kwenye
vikundi vya vijana katika halmashauri zao.
Akikabidhi
Mashine hizo Bw. Adrian kwa Mkuu wa Mkoa alisema dhumuni kubwa la shirika ni
kuwawezesha vijana kujiajili na kutoka vijiweni ili kujiunga katika vikundi na
kufanya kazi kwa kujituma na kujiingizia kipato halali.
Aidha Bw.
Adrian alisema mashine hizo zitawasaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera kujenga
nyumba za gharama nafuu kwa kutumia matofali yanayoingiliana bila kutumia
udongo yatakayofyatuliwa kwa kutumia mashine hizo za kisasa.
|
|
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera akikabidhi mashine hizo kwa Halmashauri za Wilaya alisema ili
kuhakikisha vijana wanajiajili sasa ni wakati taasisi za serikali na wananchi
binafsi kuanza kutumia matofali yatakayozalishwa kwenye vikundi hivyo vya
vijana ili kuwapa vijana ajira.
Aidha
alilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kuukumbuka Mkoa wa Kagera katika
kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, pia aliwaasa vijana kujituma na kuchapa
kazi kwa bidii ili kupata maisha bora.
Kila
Halmashauri ya Wilaya ilipewa mashine nne aidha kikundi kitakachonufaika na
mashine hizo pia kitawezeshwa shilingi 500,000/= na shirika la Nyumba la
Taifa kama mtaji wa kuanzia uzalishaji
wa tofali zenye gharama nafuu.
|
Picha/Habari Na:-
Sylvester M.
Raphael
Information
Officer
Kagera
Regional Secretariet
P.O.Box 299
Bukoba - Tanzania
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment