LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Coutinho wa Yanga SC aisaidia Timu yake kuwakung'uta Tanzania Prisons 2-1 leo Septemba 28,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 28, 2014

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Coutinho wa Yanga SC aisaidia Timu yake kuwakung'uta Tanzania Prisons 2-1 leo Septemba 28,2014.

Bao za Mbrazil, Andey Coutimho, Dakika ya 34, na Simon Msuva, Dakika ya 68, zimewapa Yanga SC ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Prisons kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa Leo Septemba 28,2014,Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa Bao 1 na Prison kumaliza wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Jacob Mwakalobo kupewa Kadi za Njano mbili na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu.

Licha ya upungufu huo, Kipindi cha Pili Prisons walisawazisha Bao katika Dakika ya 65 lakini Dakika 3 baadae Simon Msuva akafunga Bao la ushindi.

Nako huko Chamazi, Uwanja wa Azam Complex, Kagera Sugar imewachapa Wenyeji wao Bao 2-0 katika Mechi nyingine ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa hii Leo Septemba 28,2014.

Bao za Kagera Sugar zilifungwa na Salum Kanoni kwa Penati na Rashid Mandawa.
Mshambuliaji wa Yanga, Genilson Santana 'Jaja' akimpongeza mwenzake Andrew Coutinho (wa kwanza kushoto) aliyeifungia Yanga bao la kwanza dhidi ya Prisons katika Uwanja wa Taifa, Dar leo Septemba 28,2014.

Kikosi cha Prisons kilichoanza dhidi ya Yanga leo Septemba 28,2014.

MATOKEO LIGI KUU TANZANIA 2014/2015.

Septemba 27,2014.

Simba SC 1 - 1 Polisi Moro 

Azam FC 2 - 0  Ruvu Shooting 

Mbeya City 1 - 0 Coastal Union 

Mgambo JKT 0 - 1 Stand United 

Mtibwa Sugar 3 - 1 Ndanda FC

Septemba 20,2014.

Azam FC 3 - 1 Polisi Moro 

Mtibwa Sugar 2 - 0 Yanga SC

Stand United 1 - 4 Ndanda FC

Mgambo JKT 1 - 0 Kagera Sugar 

Ruvu Shooting 0 - 2 Tanzania Prisons 

Mbeya City 0 - 0 JKT Ruvu 

Septemba 21,2014.

Simba 2 - 2 Coastal Union


Kikosi cha Yanga kilichoiua Prisons ya Mbeya mabao 2-1.
MSIMAMO VPL 2014/2015.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Azam FC
2
2
0
0
5
1
4
6
2
Mtibwa Sugar
2
2
0
0
5
1
4
6
3
Mbeya City
2
1
1
0
1
0
1
4
4
Ndanda FC
2
1
0
1
5
4
3
3
5
Tanzania Prisons
2
1
0
1
3
2
1
3
6
Kagera Sugar
2
1
0
1
2
1
1
3
7
Mgambo JKT
2
1
0
1
1
1
0
3
8
Stand United
2
1
0
1
2
4
-2
3
9
Yanga
2
1
0
1
2
3
-1
3
10
Simba
2
0
2
0
3
3
0
2
11
Coastal Union
2
0
1
1
2
3
-1
1
12
JKT Ruvu
2
0
1
1
0
2
-2
1
13
Polisi Moro
2
0
1
1
2
4
-2
1
14
Ruvu Shooting
2
0
0
2
0
4
-4
0
 
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad