|
Bunduki
zilizonaswa na Polisi kutoka kwa majambazi ambao walizipora kutoka kwenye
Kituo cha Polisi cha Bushirombo wilayani Bukombe.
Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na
bunduki sita aina ya SMG, pump action tatu na mabomu 11 ya machozi.
Jeshi la Polisi nchini tayari limetangaza
dau la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha
kuwakamata au kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Geita,
limefanikiwa kulitia mbaroni jambazi moja na kufanikisha kuzinasa pamoja na
sihala hizo ambazo ziliporwa na kundi la majambazi usiku wa kumkia
Septemba 06,2014, katika kituo cha polisi wilayani Bukombe.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP),
Ernest Mangu, alisema jambazi hilo lilinaswa porini likiwa na silaha hizo
ambazo ziliporwa baada ya kuvamia kituo hicho na kuua polisi wawili papo hapo
na kujeruhi wengine wawili.
“Hawa majambazi wameonekana kujichanganya na
wafugaji waliopo mipakani, hivyo uhalifu wao wakifanya wanakimbilia kwa
wafugaji…natangaza kuanzia sasa wale wafugaji waliopo pembezoni mwa mipaka
kuondoka mara moja ili kutowapa nafasi majambazi kujificha,” alisema Mangu.
|
|
Hata hivyo,
IGP Mangu alisema baadhi ya mapori ya akiba katika mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma
na Shinyanga yamegeuzwa maficho ya wahalifu na mikakati inafanyika
kutafuta ufumbuzi wa kudumu badala ya ukanda wa mapori hayo kutangazwa kanda
maalum ya mikoa ya kipolisi.
Akikwepa kulihusisha tukio hilo la kuvamiwa kwa kituo cha polisi na kuuawa
kwa polisi wawili na kujeruhi wengine na kuondoka na silaha mbalimbali zikiwamo
bunduki aina ya SMG, risasi na mabomu ya kutupa kwa mkono, alisema matokeo ya
uchunguzi ndiyo yatabainisha ukweli halisi.
Alisema baadhi ya wahalifu hutoka nchi jirani na kushirikiana na baadhi ya
wenyeji kwa kutumia mapori ya akiba na baadhi ya hifadhi kujificha kabla
na baada ya kutekeleza uhalifu wao.
Alisema operesheni rasmi ya kuwasaka watuhumiwa waliohusika na tukio la uvamizi
wa kituo cha polisi cha Bushirombo umeanza baada ya kikao cha kamati ya ulinzi
na usalama cha mkoa wa Geita kufanyika .
|
|
Wakazi wa
mji wa vitongoji vya Bukombe mkoani Geita na maeneo jirani wakiwa katika kituo
cha Polisi Bukombe kuaga miili ya askari wawili waliouawa kwa bomu juzi usiku
baada ya majambazi kuvamia kituo hicho na kuwashambulia kisha kupora silaha.
|
Septemba
06,2014, watu wanaoaminika ni majambazi walivamia kituo cha polisi cha
Bukombe ambacho makao makuu ya polisi wilaya ya Bukombe, kushambulia na
kuwaua polisi WP 7106 Uria Mwandiga na G.2615 Pc Dustani Kimati.
Waliojeruhiwa ni E.5831 CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyeumizwa kichwa na
usoni pamoja na kung’olewa meno mawili, huku H.627 Mohamed Hassani akijeruhiwa
kifuani.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment