Picha na
Maktaba yetu……Mchungaji Samuel Sadela (114), wa Kanisa la Gospel Apostolic huko
Nigeria aliyehubiri kwa miaka 82 amefariki dunia na kuacha mjane mwenye umri wa
miaka 30 aitwaye Christina aliyemuoa miaka saba iliyopita.
Mchungaji
Sadela alioa mke wa tatu, Christina mwaka 2007, baada ya kufiwa na mke wake wa
pili mwaka 1965 ambaye alizaa naye watoto wanne na wawili kati ya hao walifariki
na mkewe huyo alifariki mwaka 2001.
Awali, Ofisa
Mwandamizi mmoja wa juu wa kanisa hilo lililopo kwenye Wilaya ya Gdagada, Lagos
aliviambia vyombo vya habari vya kimataifa kuwa, mchungaji huyo alifariki dunia
Jumapili iliyopita baada ya kuugua kidogo maradhi yanayohusishwa na uzee
kutokana na umri wake.
“Papa
(Sedela), amekufa baada ya kuugua muda mfupi, tunamkumbuka mchungaji wetu na
mlezi wa kanisa enzi za utumishi wake,” alisema Ofisa huyo ambaye hakutaka jina
lake litajwe.
Mchungaji
Sadela, alisifika sana kwa huduma yake na kusafiri maeneo mengi ndani na nje ya
Nigeria akihubiri neno la Mungu na nchi alizowahi kuhubiri ni kama vile
Marekani na Uingereza na kwamba alikuwa akisisitiza kuwa amezaliwa mwezi
Agosti, mwaka 1900, ingawa hakuna nyaraka zinazothibitisha hilo.
Taarifa
zinasema, ikiwa ni kweli mchungaji huyo amezaliwa mwaka huo, basi angekuwa
ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mujibu wa Kitabu cha Maajabu ya
Rekodi za Dunia.
Mamia ya
waombolezaji wa kanisa hilo walionesha huzuni zao huku wakijipanga kwenye
mstari mrefu kwenda kusaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kwenye viwanja
vya kanisa hilo.
Kabla ya
kuoa mke wake wa pili, Papa Sedela alikuwa na mke wa kwanza ambaye alizaa naye
watoto saba, ambao pia wote walifariki wakiwa wadogo na mkewe huyo akafa baada
ya miaka 21 ya ndoa.
Katika enzi
za uhai wake alikuwa akisema anajisikia kijana na mwaka jana alisherehekea siku
ya kuzaliwa kwake akiadhimisha miaka 113 na kusema anaamini Mungu atamuweka
aishi miaka mingi zaidi.
|
No comments:
Post a Comment